Mti wa jamii ya mchungwa

Ugonjwa wa Magome ya Michubgwa Kutoa Gundi

Phytophthora spp.

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Maeneo yenye weusi na yaliyolowa maji kwenye gome yanaanzia kwenye usawa wa udongo.
  • Gundi inayoweza kuyeyuka kwenye maji huchuruzika kutoka kwenye nyufa za gome wakati wa hali ya hewa yenye ukavu.
  • Gome chini ya udongo linakuwa limelowana, lenye utelezi na kuwa rangi ya kahawia nyekundu hadi nyeusi.
  • Maeneo yaliyokufa tishu yanaweza kuenea hadi kwenye tishu za ndani na kuzunguka gome, na hivyo kusababisha kuanguka.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Mti wa jamii ya mchungwa

Dalili

Dalili za kuoza shina mara nyingi huanza kuonekana karibu na usawa wa udongo. Maeneo yenye weusi na kulowana maji hutengenezwa kwenye gome na harufu mbaya inaweza kutokea kutokea katika hali ya majimaji. Gundi inayoweza kuyeyuka kwenye maji hutiririka kutoka kwenye nyufa za gome zilizo wima, hususani katika hali ukavu. Gome la chini ya mstari wa udongo linaweza kuwa na majimaji, linaloteleza, huku likiwa na rangi ya kahawia-nyekundu au nyeusi katika hatua za mwisho. Maeneo yenye rangi ya kahawia kutokana na kufa kwa tishu yanaweza kuenea hadi kwenye tishu za ndani za mti. Majani hubadilika rangi na kuwa ya manjano kutokana na upungufu wa virutubisho. Katika hatua za baadaye, gome lililokufa hukauka, hunywea na kutengeneza nyufa, na viraka vya shina vinaweza kuanguka, na kuacha kikwachu kilicho wazi. Miti inaweza kuanguka na kufa ikiwa kuvu (ukungu) italizunguka gome. Matunda yaliyoathirika hutengeneza uozo laini wa kahawia; uozo ambao hatimaye huzalisha harufu kali sana.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Kuweka mbegu kwenye maji ya moto (takriban nyuzi 49) kwa dakika 4-10 huondoa maambukizi yanayosababishwa na mbegu. Kuweka klorini katika mifumo ya umwagiliaji mdogo (kwa mfano umwagiliji wa vitone, wa kunyunyuzia) husaidia kwa ufanisi kupunguza maambukizi ya kuvu wa kuozesha shina. Baadhi ya aina za kuvu au bakteria (Trichoderma spp. na Bacillus spp.) zimejaribiwa kama wakala wa udhibiti wa kuvu wa kuozesha shina na zimeonyesha matokeo mazuri. Dawa za kuua kuvu za shaba zinaweza pia kutumika kudhibiti ugonjwa katika hatua za awali.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Kutibu shamba la michungwa kwa dawa za kuua kuvu zenye metalaxyl na fosetyl-aluminium ni nyongeza nzuri katika mbinu ya kinga na udhibiti wa kibaiolojia wa kuvu hawa. Matumizi ya fosetyl-aluminium kwenye majani na kutia dawa ya metalaxyl moja kwa moja kwenye udongo kuzunguka mmea, ni mbinu iliyoonyesha matokeo mazuri sana. Inapendekezwa kupulizia majani kabla ya mavuno, matibabu ya kuzamisha matunda kwenye mchanganyiko wa dawa baada ya mavuno na/au matumizi ya karatasi laini (kama vile tishu) zenye dawa zinazotumika kuzungushia machingwa.

Ni nini kilisababisha?

Dalili hizo husababishwa na aina tofauti za kuvu aitwae Phytophthora. Kuvu hawa huzalisha idadi kubwa ya vijimbegu (viiniyoga) vinavyosambazwa na maji; vijimbegu ambavyo katika hali bora kwao (unyevu mkubwa na joto la juu) vinaweza kuogelea kwa umbali mfupi. Vijimbegu hivi ndivyo visababishi vya maambukizi ambavyo vinaweza kusafirishwa na matone ya mvua au maji ya umwagiliaji hadi kwenye mizizi ya miti.Kisha, vijimbegu huota na kuingia kwenye ncha ya mizizi, na kusababisha kuoza kwa mizizi yote midogo, na baadaye kuenea kwenye mzizi mkuu. Kuoza kwa shina hutokea wakati vijimbegu hivi vinapodondokewa na matone ya maji kwenye jeraha au nyufa za gome kuzunguka kitako cha shina. Uwezekano wa miti kuathirika inategemea na aina ya kuvu waliopo kwenye eneo na inategemea zaidi na hali za mazingira zilizopo (aina ya udongo, uwepo wa maji).


Hatua za Kuzuia

  • Panda mbegu kutoka kwenye vyanzo vilivyothibitishwa.
  • Chagua aina za mbegu zenye ukinzani au zinazohistamili magonjwa kwa ajili yako la michungwa.
  • Eneo la vitalu linapaswa kuwa na mfumo mzuri wa kuondoa maji.
  • Hakikisha kwamba zana za kilimo zinatakaswa (kusafishwa kwa madawa ya kuua vijidudu) kabla ya matumizi.
  • Panda miti kwenye matuta ili kuzuia hasara kutokana na ugonjwa.
  • Epuka kujeruhi mimea, hususani karibu na kitako cha shina.
  • Ondoa sehemu za miti zilizokufa au kuathirika mara moja.
  • Kagua bustani mara kwa mara ili kubaini uwepo wa alama za ugonjwa hadi kwenye mizizi midogo ya kwanza ya pembeni.
  • Hakikisha maji ya umwagiliaji kwa njia ya mitaro hayagusani na shina kuu la miti.

Pakua Plantix