Mti wa jamii ya mchungwa

Doa la Grisi

Mycosphaerella citri

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa ya manjano ambayo hatimaye yanaweza kuwa yenye rangi ya weusi kwenye upande wa juu wa jani na kuleta vidonda vidogo kwenye upande wa chini.
  • Vidonda hugeuka kuwa vyeusi kadri vinavyokomaa na hatimaye hubadilika kutoka kuwa rangi ya kahawia hadi nyeusi.
  • Miti iliyoathirika hupoteza majani polepole, na hivyo kupunguza mavuno ya matunda.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Mti wa jamii ya mchungwa

Dalili

Dalili hutofautiana kidogo kwa ukubwa wake na muonekano kutegemeana na aina ya mti, lakini mashamba yote ya kibiashara huathiriwa kwa kiwango fulani. Dalili zinaweza kuonekana kwanza upande wa juu wa majani yaliyokomaa kama madoa ya njano hadi ya kahawia iliyokolea yanayozungukwa na eneo liilobadilika rangi na kuwa ya manjano. Malengelenge madogo ya rangi ya chungwa iliyofifia hadi kahawia ya manjano yanaweza kuonekana chini ya haya madoa kwenye upande wa chini wa jani. Baadaye dalili kwenye pande zote mbili za jani hubadilika na kuwa zenye rangi ya kahawia iliyokolea au nyeusi na kuchukua muonekano wa grisi zaidi. Miti iliyoathirika inaweza kupoteza majani polepole, kupungua uimara wa mti na mavuno ya matunda. Kwenye matunda, doa la grisi hutambulika kwa kuonekana kwa madoa madogo meusi yanayotokana na kufa kwa tishu huku yakiwa yamezungukwa na eneo la kijani, dalili inayojulikana kama doa la grisi baka la ganda gumu .Haya yanaweza kufunika sehemu kubwa ya tunda. Katika maeneo yenye joto kali na mvua nyingi, maambukizi yanaweza kutokea wakati wowote.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Samahani, hatujui tiba mbadala dhidi ya kuvu anayesababisha ugonjwa wa Doa la Grisi. Tafadhali wasiliana nasi endapo unajua mbinu yoyote ambayo inaweza kusaidia kupambana na ugonjwa huu. Tunatarajia zaidi kusikia kutoka kwako.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia pamoja na tiba za kibaiolojia ikiwa zinapatikana. Doa la Grisi kwa kawaida hudhibitiwa kwa kutumia mafuta ya petroli katika wakati mwafaka mara moja au mbili katika miezi ya joto. Hatua hii hupunguza kupenya kwa vijimbegu vya kuvu kwenye majani na matunda na hivyo kuchelewesha kuonekana kwa dalili, hata wakati ambapo vimelea tayari vimejijenga kwenye jani. Dawa zenye shaba au copper sulfate kwa kawaida huongezwa kwenye mafuta ili kufanikisha udhibiti wa dalili kwenye majani na matunda. Dawa zingine za kuua kuvu pia zimetumika hapo awali (kwa mfano strobilurins) lakini zimesababisha, kwa baadhi ya matukio, kuibuka kwa tatizo la usugu wa kuvu dhidi ya dawa hii.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa na kuvu anayejulikana kitaalamu kama Mycosphaerella citri; kuvu wanaoweza kuishi kwenye mabaki ya mazao juu ya uso wa udongo wakati ambao hakuna mazao muafaka kwao. Wakati wa majira ya kuchipua, wakati hali ni nzuri, kuvu (ukungu) huzalisha vijimbegu (viiniyoga) vinavyotawanywa na matone ya mvua, umwagiliaji wa kunyunyuzia, au umande mzito. Upepo pia unaweza kusafirisha vijimbegu hadi kwenye mashamba mengine ya machungwa. Mara vijimbegu vinapotua kwenye upande wa chini wa jani, vijimbegu hivi huota na taratibu kuvu huanza kupenya katika tishu kupitia matundu ya asili kwenye jani. Mchakato huu pia huwezeshwa na hali ya joto la juu, unyevunyevu mwingi, na kipindi kirefu cha majimaji kwenye majani. Miezi kadhaa inaweza kupita kati ya maambukizi ya awali wakati wa majira ya joto na kuonekana kwa dalili za kwanza wakati wa majira ya baridi. Kinyume chake, halijoto ya ubaridi na hali ya hewa yenye ukavu hupunguza idadi ya vijimbegu na maambukizi. Majani huendelea kuwa hatari ya kuambukizwa katika hatua zote za ukuaji wa mti ikiwa hali ya mazingira ni nzuri. Uwepo wa utitiri wa kutu kwenye miti pia ni hali inayohusishwa na ugonjwa huu.


Hatua za Kuzuia

  • Usipande miti ya jamii ya michungwa kwenye mashamba yenye historia ya ugonjwa wa madoa ya grisi.
  • Chunguza shamba ili kubaini ishara zozote za uwepo wa ugonjwa, kama vile msongamano wa matawi na majani kudondoka.
  • Epuka kutumia Umwagiliaji wa kunyunyizia/mrashi.
  • Dumisha usafi wa shamba kwa kuondoa mabaki ya mazao, majani na matunda yaliyodondoka.
  • Weka chokaa na ongeza umwagiliaji baada ya mavuno ili kuharakisha kuoza kwa majani kwenye ardhi.
  • Vinginevyo, tumia mbolea ya urea ili kudumaza ukuaji wa kuvu.

Pakua Plantix