Elsinoe fawcettii
Kuvu
Dalili hutofautiana kidogo kutegema na aina ya miti na hali ya kimazingira. Kwa kawaida, madoa madogo yaliyotota maji huonekana kwanza kwenye majani machanga. Baadaye yanageuka kuwa vidonda vyenye rangi ya krimu ya manjano au vyenye rangi angavu pande zote mbili za majani. Kadri ugonjwa unavyoendelea, vidonda hivi hubadilika na kuwa na umbo mithili ya pia (koni) isiyo na umbo maalumu, ikiwa na rangi ya kahawia, na wekundu wenye giza giza kwa juu; vidonda ambavyo vinaweza kufunika sehemu kubwa ya ubapa wa jani (lamina). Majeraha ya zamani yana vigaga/ukurutu kwa juu na muonekano wa mkwaruzo wenye nyufa na mpasuko. Majani yaliyoathiriwa yanapinda, yenye makunyanzi au mikunjo, na kingo zilizochanika. Vitawi vichanga, mashina laini, na mashina pia vinaweza kuonyesha dalili zilizo sawa. Ukuaji uliodumaa na ukuaji kama vichaka ni sifa mbili za kawaida. Wakati wa maambukizi makali, kupukutika kwa majani hutokea. Kwenye matunda, vidonda hivi vinainuka kidogo na kuwa na rangi ya waridi (pinki) hadi kahawia isiyokolea. Kadri vidonda vinapokomaa, vinakua na kurundikana sehemu moja na kuwa mithili ya magaga yenye sugu ambayo hugeuka rangi na kuwa ya kahawia ya manjano au kijivu.
Hakuna matibabu ya kibaiolojia yanayopatikana dhidi ya kuvu hawa. Dawa za kuua kuvu zilizoidhinishwa zinazotokana na shaba zinaweza kutumika kuzuia maambukizi mapya na kuenea kwa kuvu. Tahadhari inapaswa kuchukuliwa kwa sababu shaba inaweza kuwa sumu ikiwa haitatumika vizuri.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Dawa za kuua kuvu zinazotokana na thiram, difenokonazoli, na klorothalonili ambao pia zinazuia uotaji wa viinimbegu/vijimbegu, zinaweza kutumika kwa kuzuia ili kuepuka maambukizi kuenea. Dawa za kuua kuvu zinazoweza kunyonywa na mmea ni chaguo lingine. Aina za vimelea vinavyostahimili dawa za kuua aina ya kuvu vimegunduliwa.
Dalili hizi husababishwa na kuvu aitwae Elsinoe fawcettii na E. australis, ambao husababisha dalili zinazofanana katika aina tofauti za miti ya jamii ya michungwa. Mimea ya ndimu, balungi, na michenza inaathiriwa na kuvu wa aina zote mbili. Elsinoe fawcettii huathiri hasa machungwa machachu (Mdanzi au mdaranzi) na aina chache tu za machungwa matamu. Kinyume chake, E. australis husababisha ugonjwa wa makovu kwenye machungwa matamu na ndimu lakini haiathiri machungwa machachu. Rangi ya waridi hadi kahawia juu ya majani yaliyo na umbo mithili ya pia/koni kwenye majani na mithili ya tunda lenye sugu ni viinimbegu/vijimbegu vya gaga la machungwa vinavyosambazwa na matone ya mvua, umande, upepo, au umwagiliaji wa juu. Kati ya vimelea viwili vya gaga la machungwa, E. fawcettii ndiyo vilivyoenea zaidi, lakini E. australis vina athari zaidi kiuchumi kwa sababu hushambulia spishi za machungwa zinazolimwa kwa wingi.