Mti wa jamii ya mchungwa

Chule ya Michungwa

Colletotrichum gloeosporioides

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa ya rangi ya hudhurungi iliyofifia kwenye majani.
  • Katikati ya madoa hubadilika kuwa na rangi ya kijivu.
  • Madoa madogo, imara, makavu, ya kahawia hadi meusi kwenye matunda.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Mti wa jamii ya mchungwa

Dalili

Majani huoonyesha madoa ya mviringo ya rangi ya hudhurungi iliyofifia yenye ukingo wa rangi ya zambarau. Katikati ya madoa haya polepole hubadilika rangi na kuwa ya kijivu, na katika awamu za baadaye za maambukizi, yanaweza kuonyesha madoa madogo meusi yaliyosambaa. Tishu zilizojeruhiwa na sababu za kimazingira (kama vile uharibifu wa wadudu au majeraha mengine) zina uwezekano mkubwa wa kukaliwa na kuvu wa chule. Matunda ambayo yamejeruhiwa hapo awali na visababishi vingine kama vile kuchomwa na jua, kuchomwa na kemikali, uharibifu wa wadudu, michubuko, au hali mbaya za uhifadhi, yana uwezekano mkubwa wa kupata chule. Dalili za matunda ni madoa thabiti na makavu, yenye rangi ya kahawia hadi nyeusi, yakiwa na kipenyo cha milimita 1.5 au zaidi kidogo. Makundi ya vijimbegu yanayokua kwenye vidonda kwa kawaida yana rangi ya kahawia hadi nyeusi, lakini katika hali za unyevunyevu, yanaweza kubadilika na kuwa ya rangi ya waridi hadi samoni.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Dawa za kuua kuvu za kibailojia zinazotokana na Bacillus subtilis au Bacillus amyloliquefaciens hufanya kazi vizuri endapo zitatumika wakati wa hali ya hewa inayofaa. Matibabu ya mbegu au matunda kwa maji ya moto (48°C kwa dakika 20) yanaweza kuua mabaki yoyote ya kuvu na kuzuia kuenea zaidi kwa ugonjwa shambani au wakati wa usafirishaji. Dawa za kupulizia majani au matibabu ya mbegu kwa kutumia dawa za kuua kuvu zenye salfeti ya shaba zinaweza kutumika kupunguza hatari ya maambukizi.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zikiwa na hatua za kinga pamoja na tiba za kibayolojia ikiwa zinapatikana. Dawa za kuua kuvu zenye azoxystrobin au chlorothalonil zinaweza kupuliziwa mara kwa mara ili kupunguza hatari ya maambukizi. Matibabu ya mbegu kwa kutumia misombo hii pia yanaweza kuzingatiwa. Hatimaye, dawa za kuua kuvu baada ya mavuno pamoja na nta inayofaa kwa chakula zinaweza kutumika kupunguza matukio ya matunda yaliyokusudiwa kusafirishwa kwenye masoko ya nje ya nchi.

Ni nini kilisababisha?

Chule hukua kwenye matawi yaliyokufa kwenye taji la mti, na husambaa kwenye umbali mfupi kupitia matone ya mvua, umande mzito, na umwagiliaji wa kutokea juu. Kwa njia hii, chule hufikia tishu za majani machanga zinazoweza kuathirika na matunda, na kuanza kukua, na kusababisha dalili. Vikundi vipya vya vijimbegu vya chule vinazalishwa kwenye miundo ya kijinsia inayokua kwenye madoa na vidonda kwenye majani na matunda. Vijimbegu hivi vinaweza kuanza kusambaa kwa njia ya hewa na hatimae kusambaza ugonjwa kwa umbali mrefu. Mara vijimbegu vikimea, hutengeneza sehemu ya kupumzika, hapo hubaki bwete/vimelala hadi jeraha hutokea au hadi matibabu ya baada ya mavuno ya matunda (kwa mfano, kuondoa rangi ya kijani kwenye maganda ya machungwa). Hali bora kwa ukuaji wa kuvu ni unyevunyevu wa juu sana na joto la 25-28 °C, lakini kwa ujumla maambukizi yanaweza kuenea katika joto la 20-30 °C.


Hatua za Kuzuia

  • Chagua maeneo yenye mvua kidogo.
  • Panda aina za mimea zinazostahimili magonjwa na tumia mbegu zenye afya.
  • Acha nafasi ya kutosha kati ya mmea na mmea.
  • Panda miti isiyohifadhi vijidudu vya magonjwa kama vile kahawa ndani au kuzunguka shamba.
  • Pogoa miti kila mwaka ili kuboresha mzunguko wa hewa.
  • Ondoa matunda na majani yaliyodondoka kutoka shambani.
  • Safisha shamba kwa kuondoa magugu.
  • Tekeleza mbinu nzuri za mfumo wa upitishaji maji.
  • Vuna mapema ili kuepuka dalili mbaya zaidi za magonjwa.
  • Hifadhi matunda katika mazingira yenye mzunguko mzuri wa hewa.

Pakua Plantix