Mti wa jamii ya mchungwa

Baka kahawia Alternaria

Alternaria alternata

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa ya kahawia hadi meusi yenye halo za manjano kwenye pande zote za majani.
  • Baadaye, maeneo yasiyo na umbo maalumu au ya mviringo yenye seli zilizo kufa, wakati mwingine yenye uso kama karatasi iliyokakamaa.
  • Madoa meusi yenye halo za manjano kwenye matunda machanga, baadaye hufunikwa na tishu zenye magamba.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Mti wa jamii ya mchungwa

Dalili

Awali, vidonda hutokea kwenye majani machanga kama madoa madogo ya kahawia hadi meusi yenye halo za manjano, mara nyingi karibu na ukingo. Vidonda huenea katika maeneo yasiyo na umbo maalumu au ya mviringo yenye seli zilizo kufa yanayofunika sehemu kubwa ya jani. Kufa kwa seli na kubadilika kwa rangi kuwa manjano inayoweza kuenea kando ya mishipa. Vidonda ni bapa na huonekana kwenye pande zote mbili za jani. Vidonda vya zamani vina uso unaofanana na karatasi iliyo kakamaa katikati yake. Matunda ambayo hayajakomaa huonyesha madoa meusi yaliyozama kidogo yenye halo za manjano. Juu ya matunda yaliyo komaa zaidi, vidonda vinaweza kutofautiana kutoka madoa madogo hadi malengelenge makubwa. Ngozi ya matunda huunda kizuizi cha tishu za gamba ambazo zinaonekana kuwa zimetoka kwenye uso wa tunda. Ikiwa tishu za gamba zikitoka, vishimo au makovu huonekana. Kudondoka kwa matunda mapema ni kawaida.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Viuwa kuvu vya asili vinavyotokana na oksikloraidi ya shaba huonyesha matokeo mazuri dhidi ya doa kahawia la Alternaria. Iwapo unajua kitu kingine, ambacho kinaweza kusaidia kupambana na ugonjwa huu, tafadhali wasiliana nasi. Tunatazamia kusikia kutoka kwako.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Dawa za kuua kuvu zenye iprodione, chlorothalonil na azoxystrobin hutoa udhibiti mzuri wa doa kahawia la Alternaria. Bidhaa zinazotokana na propiconazole na thiophanate methyl pia zimethibitishwa kuwa zina ufanisi sana. Ni muhimu kufuata viwango maalum na kutumia dawa za kuua kuvu zenye njia tofauti za utendaji kazi ili kuzuia kutokea kwa usugu wa dawa.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa na fangasi Alternaria alternata. Huenezwa na vijimbegu vinavyo peperuka hewani kwa upepo au matone ya maji. Matukio ya mvua au mabadiliko ya ghafla ya unyevunyevu husaidia uzalishwaji na utolewaji wa vijimbegu kutoka kwa kuvu waliopo kwenye matawi, majani au madoa ya matunda. Doa/Baka kahawia la Alternaria mara nyingi huenea kati ya viunga/vitalu vyenye hifadhi za miche iliyosafirishwa na wanadamu. Kwenye majani machanga, dalili za kwanza huonekana kati ya saa 36 na 48 baada ya kuambukizwa. Matunda hubakia na uwezekano wa kuathirika kwa hadi miezi 4 baada ya kuanguka kwa petali.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia mimea yenye afya kutoka kwa vyanzo vilivyoidhinishwa.
  • Rutubisha mazao yako vizuri ili kuongeza ukinzani wa asili wa mimea, lakini epuka kuweka mbolea zenye naitrojeni kupita kiasi.
  • Weka mifereji ya kupitisha maji vizuri kwenye shamba kwani mfadhaiko wa kukosa maji au kumwagilia kupita kiasi kunaweza kusababisha kupasuka kwa matunda.
  • Epuka umwagiliaji wa juu.
  • Pendelea uingizaji hewa ya kutosha kwa kuongeza nafasi kati ya mimea.
  • Kagua mimea au mashamba yako kwa dalili za ugonjwa.
  • Pogoa matawi yaliyoathirika ili kuondoa chanzo cha vijimbegu na kupunguza maambukizi ya matunda.
  • Kusanya matunda ya zamani na matawi yaliyokufa kutoka shambani.
  • Kupembua kikamilifu na kupanga matunda kwa madaraja wakati wa kuvuna kunaweza kuzuia kuenea kwa ugonjwa wakati wa kuhifadhi na kusafirisha.

Pakua Plantix