Soya

Ugonjwa wa Ascochyta

Didymella rabiei

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa yenye unyevu kwenye majani, mashina au maganda.
  • Yanageuka kuwa ya kahawia.
  • Pete nyeusi kwenye majani.
  • Katika mashamba, mabaka ya mimea iliyoathirika yanaweza kuonekana kutoka mbali.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Soya

Dalili

Katika mimea iliyozeeka, ugonjwa huanza kama madoa yenye rangi iliyofifia na yenye unyevu kwenye majani. Baada ya muda, vidonda hivi vinakuwa vya kahawia na madoa madogo meusi huanza kujitokeza kuelekea katikati, yakitengeneza mzunguko wa pete zenye kingo nyeusi. Vidonda vilivyorefuka na kuwa na umbo la yai na rangi ya kahawia, vikiwa na madoa meusi vinaweza pia kujiunda kwenye shina. Katika hali mbaya, vidonda na madoa hulizunguka shina na hatimaye kulivunja wakati wa hali mbaya ya hewa. Madoa ya maganda yanafanana kwa muonekano na madoa ya majani. Mimea yote inaweza kuathirika, kitu ambacho huonekana kama mabaka ya kahawia kwenye shamba. Mbegu zinaweza kuambukizwa na kubeba ugonjwa hadi kwenye miche, ambao huzalisha vidonda vyeusi kahawia kwenye kitako cha shina.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Samahani, hatujui tiba mbadala dhidi ya Ascochyta rabiei. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa unajua jambo lolote linaloweza kusaidia kupambana na ugonjwa huu. Tunatarajia kusikia kutoka kwako.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi ambazo hujumuisha hatua za kinga na tiba za kibayolojia ikiwa zinapatikana. Mbegu zinaweza kutibiwa kwa kutumia madawa ya mbegu yanayotokana na thiram au thiram + thiabendazole kabla ya kupanda. Dawa za kukinga mazao dhidi ya ukungu (kwa mfano chlorothalonil) zinaweza kutumika kabla ya hatua ya maua ili kuzuia maendeleo ya ugonjwa. Mara ugonjwa unapogunduliwa, inashauriwa kutumia mzunguko wa dawa za kuua kuvu wa majani zenye mfumo wa kufanya kazi kwa kufyonzwa kwenye tishu za mmea(boscalid, mancozeb, pyraclostrobin + fluxapyroxad au bidhaa za darasa la triazolinthione). Matibabu yanaweza kuhitajika kutumiwa katika msimu wote wa ukuaji ili kuepuka hasara kubwa za mavuno.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa na kuvu/fangasi anayefahamika Didymella rabiei, ambayo hapo awali ilijulikana kama Ascochyta rabiei, na hivyo ndivyo limepatikana jina la ugonjwa. Kuvu huyu anaweza kuishi kipindi cha baridi kali kwenye mabaki ya mimea kwa miaka kadhaa. Katika hali zinazofaa, anazalisha vijimbegu vinavyoenezwa na upepo na matone ya mvua, wakati mwingine kwa umbali wa kilomita kadhaa. Hali ya hewa ya ubaridi, unyevu unyevu wa juu, umande wa asubuhi na unyevu wa majani kwa muda mrefu (saa 2 au zaidi) husaidia kuenea kwa ugonjwa. Kuvu/fangasi anaweza kukua katika joto la viwango mbalimbali (5-30°C) lakini ukuaji bora unafikiwa kati ya 15-25°C. Mizunguko mingi ya maambukizi inaweza kutokea wakati wa msimu wa ukuaji ikiwa hali ni nzuri.


Hatua za Kuzuia

  • Chagua aina za mimea inayostahimili magonjwa zaidi ikiwa inapatikana.
  • Tumia mbegu zilizothibitishwa kuwa hazina magonjwa.
  • Kinyume na hivyo, tumia mbegu kutoka shamba lenye afya.
  • Fuata mapendekezo kuhusu viwango vya mbegu.
  • Panda kwa kuchelewa ili kuepuka athari mbaya zaidi za ugonjwa.
  • Chunguza mashamba ili kuona dalili za ugonjwa mapema.
  • Ondoa mimea inayoota yenyewe na magugu ndani na karibu na shamba.
  • Vuna mapema iwezekanavyo ili kuepuka athari mbaya zaidi kwenye mazao.
  • Fuata mbinu nzuri za utakasaji shambani, kwa mfano, kuosha viatu na nguo baada ya ukaguzi wa shamba.
  • Panda dengu mara moja tu katika kipindi cha miaka mitatu kwenye shamba moja (mzunguko wa mazao).

Pakua Plantix