Uromyces ciceris-arietini
Kuvu
Mwanzoni, malengelenge ya mviringo, ya kahawia na yaliyo mithili ya unga yanaweza kupatikana pande zote mbili za majani. Kadri ugonjwa unavyoenea, madoa haya yanaweza pia kuonekana kwenye mashina na maganda. Mimea iliyoathirika inaonekana kuwa na rangi ya kahawia nyekundu.
Hadi leo hatujafahamu mbinu zozote za kibayolojia za kudhibiti ugonjwa huu. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa unafahamu kitu ambacho kinaweza kusaidia kupambana na ugonjwa huu.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye kutumia hatua za kinga pamoja na tiba za kibaiyoolojia ikiwa zinapatikana. Kudhibiti kwa kutumia dawa za kuua kuvu/ukungu kumeonyesha mafanikio kidogo. Kutu ya Dengu ni ugonjwa mdogo na mara nyingi hauhitaji hatua kali za udhibiti.
Dalili zinasababishwa na kuvu/fangasi anayeitwa Uromyces ciceri-arietini. Hali ya hewa ya baridi na yenye unyevunyevu ndiyo hali muafaka kwa kutu kwenye dengu. Mvua si muhimu kwenye maendeleo/ukuaji wa Kutu. Ugonjwa huu huonekana hasa baadaye katika msimu wa ukuaji, baada ya hatua ya utokaji wa maua.