Diplocarpon rosae
Kuvu
Dalili hujionyesha kwa madoa madogo kwenye upande wa juu wa jani. Madoa hayo ya rangi ya zambarau au nyeusi yanaweza kukua kwa kasi kutoka milimita 2 hadi 12 na kuonyesha ukingo ulioenea. Eneo la jani linalozunguka madoa hayo linaweza kugeuka manjano na kudondoka kabla ya wakati. Wakati mwingine pia mabaka madogo, meusi, yenye magamba huonekana kwenye mashina machanga. Maambukizi yakiwa makali, mmea unaweza kupukutisha/kudondosha karibu majani yote na kutoa maua kidogo.
Viambata vifuatavyo vinapendekezwa kudhibiti doa/baka jeusi la waridi: shaba, salfa ya chokaa, mafuta ya mwarobaini, baikaboneti ya potasi. Soda ya kuoka (baikaboneti ya sodiamu) pia inaweza kutumika: kijiko 1 (5 ml) kwenye lita 1 ya maji, pamoja na tone la sabuni ya maji. Mchanganyiko wenye bakteria aina ya Bacillus subtilis, unapatikana. Trichoderma harzanium iliyochanganywa na dawa za kuua kuvu pia hutoa udhibiti mzuri
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Dawa za kuua kuvu zenye tebuconazole, tebuconazole + trifloxystrobin na triticonazole zinapendekezwa ili kudhibiti doa/baka jeusi la waridi.
Madoa meusi kwenye waridi husababishwa na kuvu/fangasi aina ya Diplocarpon rosae. Kuvu hawa huishi msimu mzima kwenye majani na mashina yaliyo anguka na kuoza. Chavua/vijimbegu vya kuvu huenea kwa upepo na matone ya mvua, huambukiza sehemu wazi za majani wakati wa msimu wa mvua. Kuvu hawa hushambulia vikali zaidi wakati wa mvua na halijoto kati ya 20-26°C na hali ya unyevunyevu.