Soya

Baka Kahawia la Soya

Septoria glycines

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa ya rangi nyekundu-kahawia yenye kingo za manjano kwenye majani yaliyokomaa.
  • Madoa yanaweza kuungana, na kutengeneza maeneo makubwa ya kahawia yaliyozungukwa na halo (yaani mduara wenye mwanga) ya manjano.
  • Jani zima hubadilika kuwa na kutu ya kahawia na manjano, na kupukutika/kudondoka kabla ya wakati wake.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Soya

Dalili

Dalili za mwanzo mara nyingi huonekana kwenye majani yaliyo komaa katika sehemu ya chini ya mmea. Hali ya hewa ya joto na ya mvua wakati wa msimu wa ukuaji inaweza kupelekea dalili hizo kuenea hadi sehemu ya juu ya mmea. Madoa madogo yasiyo na umbo maalumu yenye rangi ya hudhurungi/kahawia iliyokolea hukua kwenye nyuso zote za majani, mara nyingi upande mmoja tu. Ugonjwa unapoendelea, madoa huongezeka na kuungana na kuunda maeneo ya kahawia yasiyo na umbo maalumu yenye au yasiyo na duara la mwangaza wa njano, mara nyingi huanza kwenye kingo za jani au mishipa. Baadaye, majani yote hugeuka kuwa na kutu ya kahawia na manjano, na kupukutika/kudondoka jumla. Ingawa, uharibifu sio mkubwa na mara chache husababisha upotevu wa mavuno.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Katika hali ya hewa ya mvua ya muda mrefu, tumia bidhaa zilizo na Bacillus subtilis katika hatua za mwanzo za ugonjwa huo.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Uharibifu unaosababishwa na Baka kahawia kawaida huwa mdogo. Kwa hiyo, matumizi ya dawa za kuua kuvu kwa ujumla hayashauriwi. Matibabu ya mbegu kwa dawa ya za kuua kuvu yanaweza kutumika kama kinga. Katika miaka yenye mvua nyingi, tumia dawa za kuua kuvu za kundi la azoxystrobin, chlorothalonil, mancozeb na pyraclostrobin kwenye sehemu za mimea zilizo juu ya ardhi (kwa ujumla 2-2.5 g/l ya maji).

Ni nini kilisababisha?

Baka Kahawia ni ugonjwa wa majani unaosababishwa na kuvu/fangasi wa Septoria glycines, ambao huishi kwenye mabaki ya mimea iliyoambukizwa ya msimu wa nyuma chini ya udongo. Hutokea zaidi katikati hadi mwishoni wa msimu kwani hauhusiani na mbegu. Maendeleo ya ugonjwa huu yanapelekewa na hali ya mazingira inayosaidia uwepo wa unyevu wa kila mara kwenye majani. Vipindi vya hali ya hewa ya joto kwa mda mrefu, unyevunyevu na mvua na halijoto karibu 25°C ni bora kwa ukuaji wake. Maambukizi ya kwanza hutokea wakati mvua na upepo hutawanya chavua kwenye majani ya chini. Maambukizi ya upili kati ya mmea moja na mingine pia yatatokea katika hali hizo. Hata hivyo, ugonjwa huo hupatikana hasa kwenye majani ya chini, na ikiwa hali ya hewa ni ya joto na kavu, mara chache huhamia kwenye majani ya juu. Kwa kawaida, ina athari ndogo sana kwenye mavuno.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia aina zinazostahimili magonjwa, ikiwa zinapatikana.
  • Fukia mabaki ya mimea chini kabisa ya udongo baada ya kuvuna.
  • Panga mzunguko wa mazao kama ifuatavyo mahindi, ngano, nafaka nyinginezo na alfalfa.

Pakua Plantix