Corynespora cassiicola
Kuvu
Doa lengwa ni ugonjwa unao shambulia majani zaidi. Majani huonyesha madoa ya duara hadi yasiyo na umbo maalumu yenye rangi ya kahawia-nyekundu yakiwa yamezungukwa na mduara angavu wa kijani-manjano. Ukuaji wa madoa haya mara nyingi husababisha muundo wa ukanda wa mduara wenye rangi ya kahawia nyepesi au iliyokolea, kwa hiyo kuleta jina la kawaida Doa Lengwa. Mashina na vikonyo pia yanaweza kuathiriwa na kwa kawaida kupata madoa ya kahawia iliyokolea au vidonda vilivyo refuka. Madoa meusi madogo ya duara huonekana baadaye kwenye maganda. Maambukizi makali yanaweza kusababisha majani kuanguka kabla hayajakomaa.
Hakuna tiba mbadala inayopatikana dhidi ya ugonjwa wa Doa lengwa.
Daima zingatia mbinu na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Matumizi ya dawa za kuua kuvu ni nadra sana kuwa na faida kiuchumi. Bidhaa zilizo na mchanganyiko wa pyraclostrobin, epoxiconazole na fluxapyroxad au bixafen, prothioconazole na trifloxystrobin zinaweza kusaidia kudhibiti kuvu.
Kuvu Corynespora cassiicola husalia kwa kipindi chote cha baridi kwenye vifusi vya uchafu wa mazao na kwenye udongo. Hali nzuri kwa maambukizi ni unyevu wa juu (> 80%) na unyevu wa huru kwenye majani. Hali ya hewa kavu huzuia maendeleo ya ugonjwa huu. Ugonjwa huu unaweza kuwa mbaya kwa aina zinazochelewa kukomaa au kwa aina nyepesi kushambuliwa katika misimu ya mvua nyingi.