Mbiringanya

Kuvu wa Doa-jani la Biringanya

Cercospora melongenae

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa madogo, ya mviringo, ya manjano, yaliyozama kidogo kwenye upande wa juu wa jani.
  • Madoa hupanuka na kuungana, na kuwa ya rangi ya kahawia na duara la mwanga wa manjano.
  • Kujikunja na kudondoka kwa majani.
  • Kupungua mavuno.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Mbiringanya

Dalili

Maambukizi yanaweza kutokea katika hatua yoyote ya ukuaji na yanaonekana kwenye majani, vikonyo, na mashina. Dalili za mwanzo huonekana kama madoa madogo, ya mviringo, na yaliyozama kidogo kwenye upande wa juu wa majani ya zamani, majani ya chini. Baada ya muda, madoa yanakua makubwa, yasiyo ya na umbo maalumu na yamezungukwa na duara angavu la manjano. Baadaye, madoa ya majani yanaonekana kwenye pande zote za majani. Madoa ya zamani huungana na kuchukua sifa tofauti, kutegemea na eneo lake kwenye jani. Tofauti ya sifa zao ni kuanzia kwenye rangi ya kahawia hadi rangi ya kijivu nyepesi (upande wa juu) na rangi ya kahawia nyepesi(upande wa chini). Ikiwa maambukizi ni makubwa, majani hujisokota na yanaweza kudondoka. Ingawa kuvu haambukizi matunda moja kwa moja, anaweza kusababisha kupungua kwa ukuaji wa matunda kwa sababu ya uzalishaji mdogo wa mimea.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Viumbe vya kibaiolojia vinaweza kusaidia kudhibiti maambukizi. Dawa za kibaiolojia za kuua kuvu zinazotokana na bakteria aina ya Bacillus subtilis QST 713 zinaweza kutumika kupulizia majani ili kushindana na kuvu wa doa-jani la biringanya. Mafuta ya mwarobain yanaweza kusaidia kudhibiti maambukizi, pia.

Udhibiti wa Kemikali

Mbinu jumuishi inapaswa kuzingatiwa kila wakati ili kudhibiti ugonjwa huu. Endapo dawa za kuua kuvu zinahitajika, madawa ya klorothalonil, mancozeb au asidi ya oktanoic, zikiwa katika mchanganyiko wa chumvi ya shaba zinaweza kutumika kama dawa ya kupulizia majani na kuweka kwenye udongo.

Ni nini kilisababisha?

Doa jani la biringanya ni vimelea vya kuvu wa mimea. Vijimbegu vya kuvu vinaweza kuishi kwenye mabaki ya mimea na udongo kwa angalau mwaka mmoja. Kisha huchukuliwa kwa njia tofauti kwenye majani ya chini, ya zamani. Kwa kawaida huenezwa na upepo na maji (ya mvua na umwagiliaji), lakini anaweza kutawanywa na zana za kilimo zilizoambukizwa na watu. Kisha husogea juu ya shina hadi kwenye majani machanga. Unyevu na unyevuanga wa juu ni mazingira yanayochochea maambukizi na maendeleo ya ugonjwa huo. Kwahivyo, kwa kawaida ugonjwa unatokea zaidi wakati wa msimu wa mvua (hali ya hewa ya mvua, unyevu endelevu wa mimea).


Hatua za Kuzuia

  • Panda aina za mbegu zinazostahimili au zilizo sugu dhidi ya magonjwa.
  • Tumia mbegu na zana za mmea (kama vile vipandikizi) zenye afya au zilizothibitishwa kutokuwa na vimelea vya magonjwa.
  • Dumisha nafasi iliyoongezeka kati ya mimea ili kuhakikisha kuna upitishaji mzuri wa hewa na kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.
  • Epusha/zuia ukuaji wa magugu kupita kiasi.
  • Hakikisha unarutubisha udongo kwa kiwango cha kutosha.
  • Epuka umwagiliaji wa kupita kiasi ili kupunguza unyevu na usitumie vinyunyizio vya kumwagilia maji kutokea juu.
  • Mwagilia wakati wa asubuhi kuliko jioni.
  • Epuka kufanya kazi shambani wakati mimea imelowa.
  • Ondoa au haribu mimea iliyoambukizwa na taka/mabaki kwa kuzichoma au kuzilima.
  • Inapendekezwa mzunguko wa mazao ukitumia mimea isiyohifadhi magonjwa kwa kipindi fulani.

Pakua Plantix