Mahindi

Baka la Kijivu la Jani la Mahindi

Cercospora zeae-maydis

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Vidonda vidogo sana vilivyozungukwa na duara angavu la manjano.
  • Vidonda huungana na kusababisha mabaka kwenye jani lote.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Mahindi

Dalili

Madoa madogo ya kahawia yanayotokana na kufa kwa tishu ambayo yanaweza kuwa na duara lenye mwangaza wa manjano huonekana kwenye majani ya chini, mara nyingi kabla ya maua. Polepole, vidonda hivi vitageuka rangi na kuwa vya kijivu na huonekana kwenye majani machanga. Kadiri ugonjwa unavyoendelea, vidonda huongezeka na kuwa virefu, vyenye umbo la mstatili, ambavyo hukua sambamba na mishipa ya jani. Katika hali bora (joto kali kiasi, unyevunyevu mwingi na majani yaliyolowana), vidonda hivi vinaweza kuungana na kuathiri jani zima. Ikiwa hali hii inatokea kabla ya kujaza nafaka, inaweza kusababisha upotevu mkubwa wa mavuno. Ugonjwa huu wa kuoza kwa majani unaweza kudhoofisha mimea na wakati mwingine kulainisha mashina, na kusababisha kuanguka.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hakuna udhibiti wa kibaiolojia unaopatikana kwa ajili ya kudhibiti ugonjwa huu.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Matibabu ya kupulizia majani kwa kutumia dawa ya kuua kuvu/ukungu ni njia ya kudhibiti ugonjwa ikiwa utaonekana mapema, lakini inapaswa kuzingatiwa kwa kuangalia hali ya hewa, uwezekano wa kupoteza mavuno, na uwezekano wa hatari kwa mimea. Dawa za kuua kuvu zenye pyraclostrobin na strobilurin, au mchanganyiko wa azoxystrobin na propiconazole, prothioconazole, na trifloxystrobin zinafanya kazi vizuri katika kudhibiti kuvu.

Ni nini kilisababisha?

Ugonjwa wa madoa ya kijivu kwenye majani unasababishwa na kuvu aitwae Cercospora zeae-maydis. Kuvu hawa huishi katika mabaki ya mimea kwenye udongo kwa muda mrefu. Wakati wa majira ya kuchipua, matone ya mvua na upepo hubeba vijimbegu (viiniyoga) vya kuvu hadi kwenye majani ya chini. Mzunguko wa maisha ya kuvu unawezeshwa zaidi na hali ya joto kali (25 hadi 30°C), unyevunyevu mwingi (umande, ukungu), na majani yenye maji maji kwa muda mrefu. Hali ya hewa joto kali na ukavu huzuia ukuaji wa kuvu. Dalili hutofautiana kidogo kati ya aina tofauti za mimea. Kuvu hukamilisha mzunguko wake wa maisha (kutoka kuambukiza hadi kuzalisha vijmbegu(viiniyoga vipya) ndani ya siku 14-21 kwenye aina ya mbegu zilizo kwenye hatari zaidi ya kuathirika, na siku 21-28 kwa aina ya mbegu zinazostahimili magonjwa.


Hatua za Kuzuia

  • Panda aina ya mbegu zinazostahimili magonjwa ikiwa zinapatikana katika eneo lako.
  • Panda kwa kuchelewa ili kuepuka hali mbaya kwa mimea.
  • Hakikisha kunakuwa na uingizaji mzuri wa hewa kwa kuongeza nafasi kati ya mimea.
  • Lima kwa kina kirefu na yazike mabaki yote ya mimea baada ya mavuno.
  • Panga mzunguko wa muda mrefu wa mazao kwa kutumia mimea mbadala isiyohifadhi magonjwa.

Pakua Plantix