Pamba

Ubwiri wa Kijivu wa Pamba

Mycosphaerella areola

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa madogo ya umbo pembe, yenye rangi ya kijani iliyofifia hadi ya manjano.
  • Vitu mithili ya unga mweupe kijivu hutokea chini ya madoa.
  • Madoa madogo huungana na kutengeneza madoa makubwa.
  • Majani hukauka na kuanguka kabla ya wakati, na kuacha matawi yakiwa tupu.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Pamba

Dalili

Kwa kawaida dalili huonekana kuelekea mwishoni mwa msimu wa ukuaji. Kwenye Upande wa juu wa majani ya zamani hutokea madoa madogo yenye umbo pembe, yana rangi ya kijani iliyofifia hadi ya manjano, ambayo ukomo wake ni kwenye mishipajani. Chini ya madoa upande wa chini hutokeaji vitu mithili ya unga mweupe-kijivu. Wakati wa kipindi chenye unyevunyevu mwingi, ukungu (kuvu) mweupe mithili ya rangi ya fedha hutokea kwenye pande zote mbili za jani. Majani yanayoathirika kwa kiwango kikubwa hatimae tishu zake hufa, hujikunja na kukauka, huonesha rangi ya shaba nyekundu na kudondoka kabla ya wakati. Kupukutika kwa majani husababisha mmea kudhoofika na uzalishaji wake. Majani machanga huanza kuonesha dalili. Vitumba vilivyoshambuliwa hupoteza uimara, vinafunguka kabla ya wakati au vinapasuka wakati wa kuvuna.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Matibabu ya mbegu kwa kutumia dawa zenye Pseudomonas fluorescens (10g/kg ya mbegu) yanaweza kufanywa. Kupulizia mchanganyiko wenye Vijasumu (yaani bakteria) hivi kila baada ya siku 10 kunasaidia kupunguza maambukizi kwa kiwango kikubwa. Bakteria wengine (Bacillus circulans na Serratia marcescens) wamekuwa wakitumika kudhibiti aina zingine za Ubwiri na kupunguza matukio ya magonjwa yanayohusiana na kuvu huyu kwenye mazao mengine. Mbinu nyingine ya kudhibiti ni kupulizia gramu 3 za salfa inayoweza kulowana kwenye lita moja ya maji au kumwagia kilo 8-10 za unga wa salfa kwenye hekta.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia njia jumuishi na hatua za kinga pamoja na tiba za kibiolojia endapo zinapatikana. Katika hatua za awali za ugonjwa au wakati ugonjwa bado mdogo, matibabo ya kibaiolojia hapo juu yanapaswa kuzingatiwa. Katika hatua za juu za ugonjwa au wakati ukali wa ugonjwa unaongezeka, inapendekezwa matumizi ya dawa mpya ya kuua kuvu zenye propiconazole au hexaconazole (2ml/l). Rudia matibabu baada ya wiki moja hadi siku 10.

Ni nini kilisababisha?

Dalili zinazosababishwa na kuvu ambae kwa kitaalamu hufahamika kama Mycosphaerella areola, ambae huishi kwenye mabaki ya mimea au mimea inayoota yenyewe kutokea misimu iliyopita. Hivi ndivyo vyanzo vikuu vya vijidudu vya ugonjwa katika msimu mpya. Joto kati ya 20-30 °C, hali za maji maji na unyevunyevu (asilimia 80 au zaidi) pamoja na mvua za vipindi huchochea maambukizi na maendeleo ya ugonjwa. Hali ya ubaridi ikiambatana na vipindi virefu vya usiku wenye umande kwa siku kadhaa mfululizo, hata inapotokea hakuna mvua, bado hali hizo huchochea ukuaji wa ukungu. Vijimbegu (viiniyoga) vya Ubwiri kijivu huzalishwa katika majeraha ya majani na baadaye husafirishwa na upepo hadi kwenye mimea yenye afya, na hivyo kusababisha maambukizi ya awamu ya pili. Mimea inakuwa hatarini zaidi katika sehemu ya mwisho wa msimu, kabla au wakati wa kuzalisha vitumba.


Hatua za Kuzuia

  • Panda aina ya mbegu zenye uwezo wa kuhimili ugonjwa (kuna aina kadhaa zinazopatikana).
  • Panda kwenye matuta yaliyoinuliwa ili kuboresha mfumo wa utoaji maji shambani.
  • Epuka kupanda mapema sana au kwa kuchelewa sana katika msimu.
  • Acha nafasi ya kutosha ya mmea na mmea ili kuruhusu majani kukauka haraka baada ya mvua.
  • Kagua shamba la pamba mara kwa mara ili kubaini mapema dalili za uwepo wa ugonjwa.
  • Ondoa majani yanayoonesha dalili na yateketeze.
  • Dhibiti magugu yanayoweza kuathiriwa yaliyo shambani na kuzunguka shamba.
  • Teketeza mazao yanayoota yenyewe kutokea misimu iliyopita.
  • Tumia mfumo wa umwagiliaji wa matone na epuka umwagiliaji wa kunyunyuzia (kutokea juu) ili kupunguza kulowana kwa majani.
  • Mwagilia mimea asubuhi ili yaweze kukaua wakati wa mchana.
  • Epuka umwagiliaji wa mara kwa mara ili kudumisha hali ya ukavu kwenye paa la majani (yaani kanopi) na udongo wa juu.
  • Epuka matumizi ya ziada ya mbolea zenye naitrojeni au samadi.
  • Usifanye kazi shambani wakati mimea imelowana.
  • Ondoa mabaki ya mimea na yachome mbali na shamba la pamba.
  • Tekeleza mzunguko wa mazao wa miaka 2 au 3 kwa kubadilisha na mazao yasiyohifadhi ugonjwa huu, kwa mfano mazao ya nafaka.

Pakua Plantix