Alternaria macrospora
Kuvu
Maambukizi ya mapema kwenye majani husababisha madoa madogo, yenye umbo la mviringo na rangi ya kahawia hadi hudhurungi huku yakiwa na kingo zenye rangi ya zambarau na ukubwa tofauti kuanzia kipenyo cha milimeta 1 hadi 10. Madoa haya mara nyingi huonyesha ukuaji kwa mviringo unaoleta muundo wa miduara ambayo huonekana wazi zaidi kwenye upande/ubapa wa juu wa majani. Kadri madoa yanavyokua, sehemu zao za katikati huanza kukauka na kuwa na rangi ya kijivu, na mara nyingine huchanika na kudondoka (athari ya tundu la risasi). Madoa haya yanaweza pia kuungana na kutengeneza maeneo yasiyo na umbo maalumu ambayo yamekufa katikati ya ubapa wa jani. Katika hali ya unyevunyevu, kuvu (ukungu) huzalisha na kuachia kiasi kikubwa cha vijimbegu(viiniyoga), ambavyo vinaweza kusababisha sehemu zenye vidonda kuonekana nyeusi kama masizi. Kwenye mashina, ukuaji wa vidonda huanza kama madoa madogo yaliyozama ambayo baadaye yanaweza kugeuka kuwa vikwachu (vidonda kwenye shina), kuzigawa na kuzicha tishu. Vitumba vya maua vinaweza kudondoka endapo maambukizi ni makubwa, hali ambayo hatimaye inaweza kusababisha kushindwa kwa ukuaji wa vitumba vya pamba.
Matibabu ya mbegu kwa kutumia kwa kutumia Pseudomonas fluorescens (10g/kg ya mbegu) yanaweza kutoa ulinzi wa kiasi kwa mazao. Kupulizia Pseudomonas fluorescens 0.2% kila baada ya siku 10 kunaweza kupunguza maambukizi kwa kiasi kikubwa.
Kila wakati zingatia mbinu jumuishi kwa kuchukua hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaiolojia endapo yanapatikana. Kwa kawaida, ugonjwa huu haupunguzi mavuno kwa kiwango kinachohitaji matibabu maalum ya dawa za kuua kuvu. Katika uambukizaji mkubwa, dawa za kuua kuvu kama vile maneb ambayo ina mancozeb (2.5 g/l), hexaconazole (1 ml/l), tebuconazole, na difenoconazole zinaweza kutumika kudhibiti madoa ya majani ya Alternaria. Matibabu ya mbegu kwa kutumia strobilurins (kwa mfano trifloxystrobin) au vizuizi vya usanisi wa steroli (kwa mfano triadimenol, ipconazole) yanaweza kutumika kufanya mbegu ziwe na kinga dhidi ya vimelea.
Dalili hizi husababishwa na kuvu aitwae Alternaria macrospora, ambae husalia kwenye mabaki ya pamba endapo hakuna tishu zilizo hai au mimea mbadala wanamoweza kuishi. Mgonjwa huu huenea kupitia mbegu zinazosambazwa hewani na matone ya maji yanayopiga mimea yenye afya. Uzalishaji wa mbegu ndani ya madoa ya majani pamoja na mchakato wa maambukizi unachangiwa na hali ya hewa yenye unyevunyevu na joto la takriban 27 °C. Mimea huwa katika hatari kubwa zaidi wakati wa hatua ya miche na mwishoni mwa msimu wakati majani yanaanza kunyauka. Hatari ya maambukizi hupungua kutoka majani ya chini hadi ya juu ya pamba. Katika hali zinazofaa kwa kuvu, aina za pamba zinazoweza kuathirika zinaweza kupukutisha majani kwa haraka, hususani pale ambapo kitumba cha kikonyo kinapoambukizwa. Ukuaji wa dalili unachangiwa zaidi na athari za kifiziolojia au lishe kwa mmea, kama vile mzigo mzito wa matunda au kuzeeka kwa mmea kabla ya wakati.