Phakopsora pachyrhizi
Kuvu
Maambukizi huanza katika sehemu za chini za mmea na kisha kuelekea juu, na kuathiri hasa majani machanga. Dalili za mwanzo huonekana kwenye hatua ya mmea kutoa maua kwa namna ya matundu madogo sana yenye rangi ya ugoro/kahawia iliyokolea kwenye upande wa chini wa majani, mara nyingi kwenye mishipa. Baadaye, madoa haya huongezeka kwa ukubwa na idadi na kuwa na rangi nyekundu kahawia au nyeusi. Ugonjwa unapoendelea, hufunikwa na upele kuvu wa kahawia iliyo pauka unao onekana kwa macho. Baadhi ya upele huo huungana na kutengeneza madoa ya kahawia iliyokolea yasiyo na umbo maalumu yakizungukwa na halo ya manjano. Sasa yana kuwepo pande zote mbili za jani, mara chache huwepo kwenye vikonyo vya majani na shina. Upukutishaji mapema wa majani unaweza kutokea.
Tumia bidhaa zenye mafuta muhimu ya Corymbia citriodoria kwa 1%, Cymbopogon nardus kwa 0.5%, na Thymus vulgaris kwa 0.3% ili kupunguza ukali wa maambukizi.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Ni muhimu kuchagua dawa inayofaa na kuitumia kwa wakati sahihi. Tumia dawa za kuua kuvu zenye hexaconazole (2 ml/lita ya maji) na propiconazole (1 ml/lita ya maji). Tumia michanganyiko ya madini ya zinc iron-maneb complex kwa vipindi tofauti katika msimu mzima.
Kutu ya soya ni ugonjwa mkali unaosababishwa na kuvu/fangasi aina ya Phakopsora pachyrhizi. Hawaambatani na mbegu na huhitaji tishu hai za kijani ili kuishi na kukamilisha mzunguko wake wa maisha. Wakati hakuna mimea ya soya karibu, huhitaji mwenyeji mbadala ili kuishi. Chavua zinazozalishwa kwenye vipele huruka kutoka mmea mmoja hadi mwingine na kupenya kwenye seli za mmea moja kwa moja, badala ya kupitia kwenye matundu au majeraha kwenye tishu za majani. Maendeleo ya ugonjwa huu huchangiwa na kuwepo kwa unyevu nyevu wa majani mfululizo kwa mda wa masaa 6 hadi 12, jotola wastani (16 hadi 28°C) na unyevu wa juu (>75%).