Mahindi

Kutu ya Kusini ya Mahindi

Puccinia polysora

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Vidonda vidogo, mithili ya poda au unga unga, vyenye rangi nyekundu-machungwa, vikiwa vimekusanyika kwa wingi kwenye upande wa juu wa jani.
  • Mabaka ya manjano na kahawia pia huonekana kwenye majani.
  • Ugonjwa huu husababisha kuoza kwa shina, mimea kuanguka, na ubora duni wa nafaka.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Mahindi

Dalili

Ugonjwa wa Kutu Kawahia ya Mahindi huonekana kama vidonda vidogo mithili ya ncha ya pini, vyenye rangi ya machungwa-nyekundu kwenye upande wa juu wa majani ya zamani, na vikiwa vichache kwa upande wa chini. Vidonda hivi vipo mithili ya poda, umbo la mviringo hadi la yai, vikiwa vimeinuka na kujirundika kwa makundi. Katika hatua za baadaye za ugonjwa, vidonda hivi hutawanyika kwa wingi na vinaweza pia kuonekana kwenye majani machanga, vifuko vya majani (vijalizo), maganda, na mashina. Mabaka yaliyobadilika rangi na kuwa ya manjano na ya rangi ya kahawia (kutokana na kufa tishu) pia huonekana kwenye majani. Majani machanga yanaathirika zaidi kuliko majani ya zamani, na kufanya mashamba yaliyopandwa kwa kuchelewa kuwa hatarini zaidi kuathirika. Afya duni ya mimea husababisha kuoza kwa shina, mimea kuanguka, na nafaka zenye ubora duni. Uwezo wa ugonjwa huu kuenea unaweza kusababisha hasara kubwa ya mavuno.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Tumia maji maji ya mmea wa guaco (Mikania glomerata- jamii ya mimea inayotambaa) ili kuzuia kuota kwa vijimbegu vya kuvu. Majimaji haya yanaweza kuandaliwa kwa kuzamisha majani yote ya guaco kwenye maji yaliyotoneshwa (yanayotokana na mvuke) na kuweka mchanganyiko wake kwenye friji kwa saa 24. Baada ya hapo, chuja mchanganyiko huo kwa kutumia karatasi ya kuchujia, uzimue kwenye maji hadi ukoleaji (concentration) wake ufike 5% na kisha utumie kwenye majani.

Udhibiti wa Kemikali

Ni muhimu kuzingatia mbinu jumuishi zenye kinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia yanayoweza kupatikana. Dawa za kuua kuvu haziwezi kuponya sehemu za mimea zilizoathirika, hivyo zinaweza tu kutumika kama hatua ya kinga ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo kwenye mimea yenye afya na kuzuia kuenea kutoka mmea mmoja hadi mwingine. Ni muhimu pia kutumia dawa hizi kwa wakati sahihi, huku ukizingatia umri wa mmea, kiwango cha ugonjwa, na hali ya hewa. Dawa za kuua kuvu zinazotokana na mancozeb, cyproconazole, flutriafol + fluoxastrobin, pyraclostrobin, pyraclostrobin + metconazole, azoxystrobin + propiconazole, na trifloxystrobin + prothioconazole zinaweza kupunguza kwa ufanisi athari za ugonjwa. Mfano mmoja wa matibabu unaweza kuwa: Kupulizia mancozeb kwa kiwango cha 2.5 g/l mara tu vidonda vinapoonekana na kurudia kila baada ya siku 10 hadi wakati wa kutoa maua.

Ni nini kilisababisha?

Ugonjwa wa Kutu Kawahia ya Mahindi husababishwa na kuvu (fangasi) anayefahamika kama Puccinia polysora, na kwa kawaida huathiri mimea katika hatua za baadaye za ukuaji katika maeneo ya kitropiki hadi nusutropiki. Kuvu huyu ni kijidudu ambacho hakiwezi kukamilisha mzunguko wake wa maisha bila kupata mmea hai anamoweza kuishi, ikiwa na maana , hawezi kuishi kwenye mabaki ya mimea, udongo au mbegu. Hivyo basi, maambukizi katika msimu mmoja hayamaanishi kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi mengine katika msimu unaofuata. Vijimbegu (viiniyoga) vya kuvy vinavyopeperushwa na upepo kutoka kwenye mashamba au maeneo mengine ndio chanzo kikuu cha maambukizi. Ugonjwa huo kisha huenezwa kwa njia ya upepo au maji kutoka mmea hadi mwingine. Hali bora inayochochea maambukizi makubwa ni joto kati ya nyuzi joto 27°C na 33°C na kiwango cha juu cha unyevunyevu. Maambukizi ya mapema katika msimu wa ukuaji yanaweza kusababisha uharibifu mkubwa na wa haraka wa mimea.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia aina za mahindi zinazostahimili au kuvumilia ugonjwa ambazo zinapatikana katika eneo lako.
  • Epuka kupanda mahindi mwishoni mwa msimu.
  • Kagua shamba mara kwa ili kubaini ishara zozote za ugonjwa.
  • Hakikisha mbolea inatumika kwa uwiano sahihi ili kuimarisha mimea.
  • Epuka kumwagilia maji kupita kiasi wakati wa hatua za mwisho za ukuaji.

Pakua Plantix