Shayiri

Doa Nyavu

Pyrenophora teres

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa ya kahawia yanayoonekana kama matundu kwenye majani, yakitengeneza muundo mithili ya wavu au chandarua.
  • Vidonda hukua kwenye sehemu mbalimbali za jani, vikiwa vimezungukwa na mduara wa mwanga wa manjano.
  • Michirizi midogo ya kahawia kwenye "ganda".
  • Mbegu zilizonyauka.

Inaweza pia kupatikana kwenye

2 Mazao
Shayiri
Ngano

Shayiri

Dalili

Doa Nyavu lina muundo wa aina mbili: muundo wa doa na muundo wa wavu. Dalili huonekana zaidi kwenye majani, lakini mara moja moja zinaweza pia kuonekana kwenye kifuko cha majani na ganda la mbegu. Umbile la wavu huanza kama vidonda vidogo vya kahawia ambavyo hurefuka na kutoa mistari miembamba, ya kahawia iliyokolea ambavyo hupishana (mithili ya nyuzi za nyavu) kwenye ubapa wa jani na hivyo kutengeneza muundo wa kipekee ulio mithili ya wavu. Vidonda vya zamani huendelea kurefuka sambamba na mishipa ya majani na mara nyingi huzungukwa na ukingo wa manjano. Mwanzoni, madoa ni madogo, ya mviringo na yenye rangi ya kahawia, yakiwa yamezungukwa na kingo za manjano. Baadaye, madoa haya madogo huongezeka ukubwa na kuwa madoa ya wavu (net blotch) yenye rangi ya kahawia iliyofifia hadi iliyokolea na kipenyo cha mm 3-6. Masuke yanaweza kuambukizwa vilevile. Michirizi midogo ya kahawia, isiyo na muonekano wa wavu, hujitokeza kwenye glume, na hivyo kusababisha mavuno kupungua na mbegu kukauka. Punje za shayiri zilizoambukizwa zina madoa ya kahawia yasiyo dhahiri kwenye sehemu zao za chini.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Samahani, hatujui njia mbadala ya tiba dhidi doa nyavu. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa unafahamu jambo lolote linaloweza kusaidia kupambana na ugonjwa huu. Tunatarajia kusikia kutoka kwako.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia ikiwa zinapatikana. Dawa za kuua kuvu zenye triazole na strobilurin ambazo hutumika kwa kupulizia majani ni bora katika kudhibiti aina zote mbili za Doa Nyavu. Epuka kutumia tebuconazole. Katika mazingira yenye mvua nyingi, inaweza kuwa muhimu kupulizia mara mbili. Kadri iwezekanavyo, zungusha dawa za kuua kuvu (ukungu) zenye mitindo tofauti ya utendaji kazi, ambayo itapunguza hatari ya kutokea ukinzani. Kutibu mbegu ndio njia pekee iliyo bora dhidi ya doa nyavu.

Ni nini kilisababisha?

Madoa ya wavu, yaani Net blotch husababishwa na kuvu (ukungu) anayefahamika kitaalamu kama Pyrenophora teres. Kuvu hawa huishi msimu mzima wa baridi kwenye mabaki ya mazao na mimea inayoota yenyewe. Ugonjwa pia unaweza kuanzia kwenye mbegu zilizoambukizwa, ingawa mara nyingi kwa kiwango kidogo. Ugonjwa huu huenea kupitia vijimbegu (viiniyoga) vya kuvu ambavyo hubebwa na upepo na rasharasha za mvua. Maambukizi ya kwanza ya mazao hutokea baada ya takriban saa sita za hali ya unyevu katika joto kati ya 10ºC na 25ºC. Ueneaji wa vijimbegu vya kuvu kwa njia ya upepo hutokea siku 14 hadi 20 muda wowote baada ya maambukizi ya kwanza hali inapokuwa muafaka. Maambukizi makubwa hupunguza eneo la kijani kwenye jani na vile vile hupunguza tija za mimea, na yanaweza kusababisha majani kufa kabla ya wakati. Kuvu pia kukua ndani ya shina. Baada ya mavuno kuvu huishi kwenye mabua yaliyoachwa, ambapo maambukizi mapya yanaweza kuanza msimu unaofuata. Ugonjwa wa Net blotch hasa hasa husababisha kupungua kwa uzito wa mbegu na ubora wa nafaka.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia mbegu kutoka kwenye mimea yenye afya au kutoka kwenye vyanzo vilivyothibitishwa kutokuwa na vimelea vya magonjwa.
  • Tumia aina za mbegu zinazostahimili magonjwa ikiwa zinapatikana.
  • Panda kwa kuchelewa katika msimu ikiwa inawezekana.
  • Wakati wa kupanda, kitalu kinapaswa kuwa na uvuguvugu, unyevunyevu na mfumo mzuri wa utoaji maji.
  • Usipande mbegu kwenye shimo lenye kina krefu zaidi kuliko inavyohitajika ili kutoa unyevu wa kutosha kwa mbegu.
  • Hakikisha kuna virutubisho vya kutosha.
  • Hakikisha udongo una kiwango cha kutosha cha Potasiamu.
  • Fuatilia mimea kwa ukaribu wakati wa kuibuka kwa jani la mwisho.
  • Fanya mzunguko wa mazao na mazao mengine yoyote, inaweza kuhitajika kupumzisha shamba kwa miaka miwili.
  • Dhibiti nyasi na mazao yanayoota yenyewe.
  • Lima kwa kuchimbua ili kufukia mabaki ya mimea chini ya ardhi baada ya kuvuna.
  • Punguza mabaki ya mabua kwa kadri inavyowezekana.

Pakua Plantix