Nyingine

Kuvu Rhynchosporium

Rhynchosporium secalis

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Vidonda vyenye rangi ya manjano, visivyo na mpangilio au vya umbo la almasi huenea kwenye majani yaliyo zeeka.
  • Katikati ya vidonda hukauka na kufifia huku kingo zikigeuka kahawia.
  • Vidonda hukua na kuungana kufunika maeneo makubwa ya jani.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao
Shayiri

Nyingine

Dalili

Maambukizi ya ya kuvu wa Rhynchosporium yana sifa ya vidonda vya kipekee vinavyojitokeza kwenye coleoptiles(ala zinazolinda ncha za machipukizi/matawi machanga), majani, ala za majani, glumes, bracts za maua, na mshuke. Dalili za kwanza huonekana kama vidonda vya manjano, visivyo na umbo maalumu au vyenye umbo la almasi (1 -2sm) kwenye lamina (sehemu bapa ya jani) au kwapajani (yaani, sehemu iliyo kati ya kikonyo cha jani na shina) za majani ya zamani. Kisha, vidonda hivi hubadilika na kuwa na rangi ya kijivu yenye mwonekano wa majimaji. Baadaye, katikati ya vidonda hukauka na kufifia, hubadilika na kuwa na rangi ya kijivu hafifu, hudhurungi (kahawia ya manjano) au nyeupe. Kingo zake zinakuwa za kahawia iliyoiva na zinaweza kuzungukwa na duara la mwanga wa manjano. Vidonda vinapokua, huungana na kuwa na umbo la yai hadi umbo mithili ya mstatili, bila kupunguzwa na mishipa ya majani. Majani machanga na maua pia yanaweza kuambukizwa ikiwa maambukizi ni makubwa au katika hatua za baadaye. Maambukizi ya maua yana sifa ya vidonda ambavyo katikati vina rangi ya hudhurungi iliyofifia na kingo za kahawia iliyoiva karibu na kitako cha shuke.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Samahani, hatujui tiba mbadala dhidi ya kuvu aina ya Rhynchosporium secalis. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa unajua chochote kinachoweza kusaidia kupambana na ugonjwa huu. Tunatarajia kusikia kutoka kwako.

Udhibiti wa Kemikali

Wakati wote zingatia mbinu jumuishi za usimamizi wa wadudu, ikiwa ni pamoja na hatua za kinga pamoja na tiba za kibayolojia ikiwa zinapatikana. Matibabu ya mbegu kwa kutumia dawa za kuua kuvu yanaweza kusaidia kupunguza uwezekano wa mlipuko wa mwanzoni mwa mwa msimu. Tumia mchanganyiko wa dawa za kuua kuvu na mitindo tofauti ya utekelezaji kutoka kwa madawa ya kundi la strobilurin na anilinopyrimidine.

Ni nini kilisababisha?

Rhynchosporium ni kuvu anaesambazwa kwa njia ya mbegu, ambae pia anaweza kuishi hadi mwaka mmoja kwenye mabaki yanayohifadhi magonjwa ambayo yameambukizwa, na haya ni kama vile mabaki ya shayiri au mimea inayoota yenyewe. Viinimbegu husambazwa kwa umbali mfupi na matone ya mvua na kwa kiwango kidogo kwa njia ya upepo. Utengenezwaji wa vijimbegu vya kuvu na maambukizi vinaweza kutokea katika joto la kati ya 5°C na 30°C. Mazingira rafiki zaidi ni joto la kati ya 15°C na 20°C na masaa 7 hadi 10 ya unyevunyevu wa majani. Dalili huonekana kwanza na zinakuwa kali zaidi katika hali za joto la juu. Ikiwa jani bendera (jani la mwisho kutoka) na majani mawili ambayo moja kwa moja yapo chini yake (ya jani bendera) yanathirika, matokeo yake ni kupungua kwa mavuno. Ikiwa kuna maambukizi yaliyofichika (yaani yasiyoonesha dalili), vimelea vya magonjwa vinaweza kuishi katika mabaki ya mimea kutoka msimu mmoja hadi mwingine.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia aina za mbegu zinazostahimili ugonjwa zinazopatikana katika eneo lako.
  • Kuchelewa upandaji wa shayiri ya majira ya baridi na ngano nyekundu ya majira ya baridi.
  • Udhibiti wa magugu ndani na kuzunguka shamba.
  • Kagua mimea au mashamba ili kugundua dalili zozote za ugonjwa wakati hali rafiki kwa kuvu zinapokuwepo.
  • Fanya kilimo cha mzunguko na mazao yasiyobeba magonjwa.
  • Lima kwa kina ili kufukia mabaki ya mimea chini ya uso wa ardhi.

Pakua Plantix