Fusarium graminearum
Kuvu
Ukali wa dalili hutegemea aina ya mazao (maimea mwenyeji ni ngano, oti na shayiri), wakati wa maambukizi na hali ya mazingira. Ugonjwa huo una sifa ya kuwa na aina mbili za dalili: Baka la miche na baka la suke. Awali, vidonda vya kahawia nyepesi, vilivyolowa maji huonekana kwenye kitako cha shina na miche hugeuka kuwa tishu zilizo kufa wakati wa kuota. Hii hushambulia zaidi wakati mbegu zilizo ambukizwa zimepandwa kwenye udongo wenye baridi na unyevu. Katika hatua za baadaye za ukuaji wa mmea, kuoza kwa taji na kitako cha shina huzingatiwa. Masuke yaliyo lowa maji na rangi ya majani iliyopauka ni ishara mbili tofauti za ugonjwa wa baka la suke. Wakati wa hali ya hewa ya joto na unyevunyevu, mabaka hayo huchukua rangi ya waridi hadi kahawia-nyepesi, kutokana na ukuaji mwingi wa kuvu. Punje zina mwonekano uliosinyaa na mbaya. Kawaida, maambukizi huenea kutoka kwa punje hadi punje mpaka suke zima linathiriwa. Katika baadhi ya mazao, hasara ya mavuno imetathminiwa hadi 70%.
Mawakala kadhaa wa udhibiti wa kibayolojia wamejaribiwa kwa mafanikio ili kupunguza athari za maambukizi ya Fusarium graminearum. Katika ngano, bidhaa mbalimbali zilizo na bakteria Pseudomonas fluorescens, Bacillus megatherium na Bacillus subtilis zimetumika wakati wa maua ili kupunguza matukio ya ugonjwa huu, ukali wake na hasara za mavuno. Mengi ya majaribio haya yalifanywa katika hali iliyodhibitiwa na faili. Fangasi washindani Trichoderma harzianum na Clonostachys rosea pia wametumiwa kwa mafanikio fulani. Matibabu ya joto kavu la 70 ° C kwa siku 5 ilionekana kuwa njia ya ufanisi ya kuondoa kuvu huyu kutoka kwenye mbegu, pamoja na wengine, kutoka kwenye mbegu za ngano na shayiri.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia, ikiwa yanapatikana. Kupangilia mda wa uwekaji wa dawa ya kuua kuvu ni muhimu kwa udhibiti wa baka fusari la suke. Kunyunyizia majani wakati wa maua na dawa za kuua kuvu za familia ya triazole (metconazole, tebuconazole, prothioconazole na thiabendazole) husababisha kupunguza kwa kiasi kikubwa matukio ya ugonjwa huo na kiasi cha mycotoxin kwenye nafaka. Kumbuka kuwa kuna vipindi vya zuio la kuvuna kwa bidhaa hizi.
Dalili za baka la suke la nafaka husababishwa na kuvu Fusarium graminearum, ambayo huishi kati ya misimu katika mimea ambayo ni mwenyeji mbadala au katika hali ya kujificha kwenye uchafu wa mazao na viumbe hai kwenye udongo. Wakati wa hali nzuri, huanza kutoa vijimbegu ambavyo vinaweza kusafirishwa na mikondo ya hewa kwa umbali mrefu. Inafikiriwa pia kuwa kuenea kwake kunaweza kuwezeshwa na aina fulani za mbu wa usubi. Uwezekano wa nafaka kushambuliwa na kuvu hiyu ni wa juu zaidi karibu na kipindi cha maua. Mara tu anapoota kwenye tishu za mmea, ana uwezo wa kupenya ngozi ya juu moja kwa moja kupitia vitundu vya asili. Anapokua katika tishu za mishipa, huzuia usambazaji wa maji na virutubisho kwenye masuke, na kusababisha punje zilizopauka na kusinyaa. Aidha, uzalishaji wa sumu hupunguza soko la nafaka. Aina mbalimbali za vipengele vya kimazingira kama vile mwangaza, halijoto, unyevunyevu, mvua na unyevunyevu kwenye majani vinaweza kuathiri mzunguko wa maisha yake. Joto kati ya 20-32 ° C na unyevu wa muda mrefu wa majani ni rafiki sana.