Zymoseptoria tritici
Kuvu
Dalili za awali za doa la septoria tritici ni madoa madogo ya yaliyobadilika rangi kwenye majani ya chini ambayo huonekana punde tu baada ya miche kuota. Yanapo tanuka, madoa haya huwa na rangi ya kahawia nyepesi hadi kahawia iliyokolea yenye umbo la mviringo au mchirizi unaoweza kuambaa kwenye ubapa wa jani. Pia huonekana kwenye mashina na masuke, hata hivyo kwa kiasi kidogo. Miundo myeusi inayotoa matunda ndani ya madoa huipa mwonekano wa madoadoa. Baadaye, majani yote yanaweza kumezwa na vidonda vyenye kutu ya rangi ya kahawia na visiwa vya tishu za kijani kibichi pekee hubakia, vimezungukwa na halo ya manjano. Hatimaye, majani hukauka na kufa. Kwa kukosekana kwa miundo myeusi inayotoa matunda, dalili zinazofanana za madoa zinaweza kusababishwa na ugonjwa mwingine au shida ya lishe kama vile sumu ya aluminiamu au upungufu wa zinki. Dalili huonekana kwanza katika hatua za baadaye za ukuaji wa mmea, wiki mbili hadi tatu baada ya kuambukizwa.
Mawakala wa udhibiti wa kibaolojia wametumika kwa mafanikio dhidi ya M. graminicola katika hali zilizodhibitiwa. Fangasi wa kundi la Trichoderma na baadhi ya spishi za pseudomonads na bacillus zimeonyeshwa kulinda mimea ya ngano dhidi ya magonjwa ya madoa kwenye majani au kuzuia kuendelea kwa ugonjwa.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Makundi mengi ya M. graminicola yametengeneza ukinzani kwa haraka dhidi ya viua kuvu, hasa kwa kundi la kemikali la strobilurin. Kiwango sahihi cha kiuchumi kinategemea upotevu wa mavuno unaotarajiwa, thamani ya soko la ngano na gharama za uwekaji wa dawa ya kuua kuvu. Dawa za kuua kuvu za kikundi cha azole hutumiwa kwa kawaida kama dawa ya kupulizia majani. Dawa mbadala za kuua kuvu kama vile carboxamide au benzophenone husaidia kupunguza ukuaji wa ukinzani.
Ugonjwa huu husababishwa na fangasi Mycosphaerella graminicola. Husalia kwenye uchafu wa mimea juu ya uso wa udongo, katika mimea ya nyasi, katika mimea iliyoota yenyewe na katika mazao yaliyopandwa msimu wa vuli. Vijimbegu husambazwa kupitia mvua na upepo kwa umbali mrefu. Dalili za mwanzo huonekana kwenye majani yaliyozeeka na mbegu zinavyotawanyika kuelekea juu, vidonda huanza kuonekana kwenye majani ya juu. Ikiwa jani la juu kabisa na majani mawili ya chini yake yameathiriwa, kupungua kwa mavuno hutokea. Mzunguko wa maisha ya Kuvu huchukua siku 15 hadi 18 kukamilika, kulingana na hali ya joto. Hali bora ni joto kati ya 15 ° C na 25 ° C na maji yanayoelea au unyevu wa juu wa muda mrefu. Chini ya 4 ° C mzunguko wa maisha hsimamishwa. Kwa maambukizi yenye mafanikio, angalau masaa 20 ya unyevu wa juu ni muhimu. Majira ya mvua na majira ya joto ni bora.