Puccinia substriata
Kuvu
Madoa ya manjano hadi meupe yaliyoinuka huonekana pande zote mbili za jani. Kadri ugonjwa unavyoendelea, madoa huungana na kutengeneza malengelenge yenye mithili ya rangi nyekundu-machungwa na kutu. Malengelenge yanaweza kuwa na kingo za manjano na yanaweza kubadilika na kuwa na rangi nyeusi katika hatua za baadaye. Majani yanaweza kufa kutokana na maambukizi na katika hali mbaya, mimea huanguka. Ugonjwa unaweza kutokea katika hatua yoyote ya zao, lakini hasara kubwa itatokea ikiwa maambukizi yatatokea kabla ya kutoka maua.
Aina za kuvu/ukungu kama Azadirachtin 0.15% au Trichoderma viride 3% zinaweza kupuliziwa kudhibiti ugonjwa wa kutu. Kinyume na hapo, Aspergillus globosum, Chaetomium globosum, na Trichoderma koningii pia zinaweza kutumika.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kukinga magonjwa pamoja na matibabu ya kibaiolojia, ikiwa yanapatikana. Kwa wakulima wadogo, dawa za kuua kuvu mara nyingi hazina tija. Hata hivyo, dawa za kuua kuvu kama misombo ya shaba, Chlorothalonil, salfa au Mancozeb zinaweza kutumika kudhibiti kutu kwenye uwele.
Dalili hizi husababishwa na kuvu Puccinia substriata. Kuna wigo mpana wa mimea inayobeba vimelea vya ugonjwa huu, na mimea hii ni kama vile biringanya na aina nyingi za nyasi. Kimelea kinaweza kusambazwa kwa umbali mrefu kwa njia ya upepo. Zaidi ya hayo, kimelea hiki huishi kwenye udongo, mabaki ya mimea, na kwenye mimea mbadala inayobeba/inayohifadhi vimelea hivi. Hali zinazofaa kwa kuvu huyu ni usiku wenye baridi (15-20°C) na mchana wenye joto (25-34°C), hali ambayo huwezesha umande kutokea kwenye majani. Hii huongeza hatari ya maambukizi.