Pilipili Hoho & Pilipili

Doajani Cercospora la Pilipili

Cercospora capsici

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa makubwa ya kahawia iliyokolea kwenye majani yenye kitovu cheupe, miduara myeusi na halo ya manjano ('jicho la chura').
  • Madoa huongezeka na kuwa vidonda vikubwa.
  • Majani yanageuka manjano na kudondoka, na kuyaanika matunda kwenye jua.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Pilipili Hoho & Pilipili

Dalili

Katika hatua ya awali ya maambukizi, madoa ya mduara ya rangi ya kahawia yenye rangi ya kijivu nyepesi katikati na kingo za kahawia nyekundu huonekana kwenye majani. Baadaye, hukua na kuwa madoa makubwa ya mviringo ya rangi yahudhurungi, yenye ukubwa wa hadi 1.5 cm, ambayo hutengenezwa na miduara myeusi yenye kitovu cha pamoja inayokua karibu na kitovu cheupe. Miduara myeusi na miduara angavu ya njano huyapa madoa mwonekano wa 'jicho la chura'. Madoa yanapozidi kuongezeka, huungana polepole na kutengeneza vidonda vikubwa vya majani. Kitovu cheupe mara nyingi hukauka na kumeguka, na kuacha athari ya 'shimo la risasi'. Katika hatua za baadaye za maambukizi, majani yanageuka manjano na kunyauka au kuanguka, na kuanika matunda kwenye jua. Katika hali mbaya, madoa yanaweza pia kuonekana kwenye kijitawi cha matunda na calyx, mara nyingi husababisha kuoza kwa shina.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Matibabu ya mbegu kwa maji ya moto ya 52 ° C kwa dakika 30 ni njia ya kupunguza uwepo wa kuvu kwenye mbegu. Kumbuka kwamba matibabu yanaweza pia kuathiri kuota kwa mbegu ikiwa hayatafanywa vizuri (muda au joto kupita kiasi). Kunyunyizia majani kwa bidhaa zenye copper hydroxide kunaweza kufanywa, kuanzia wakati madoa yanapoonekana, na kuendelea kwa muda wa siku 10-14 hadi wiki 3-4 kabla ya mavuno ya mwisho. Ni muhimu kunyunyiza pande zote mbili za majani.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Matibabu ya mbegu na captan (3g/kg) hufanya kazi vizuri katika kupambana na ugonjwa huo. Matibabu mengine ya kudhibiti ugonjwa huu ni pamoja na dawa ya kunyuzia majani ya bidhaa zenye copper hydroxide, klorothalonil au mancozeb. Matibabu yanapaswa kuanza wakati madoa yanapoonekana kwa mara ya kwanza na kuendelea kwa muda wa siku 10-14 hadi wiki 3-4 kabla ya mavuno ya mwisho. Ni muhimu kunyunyiza pande zote mbili za majani.

Ni nini kilisababisha?

Dalili hizo husababishwa na kuvu aina ya Cercospora capsici, ambayo hustahimili hasa katika ukanda wa tropiki, na huathiri mimea katika vitalu vya mbegu na mashambani. Anaishi kutoka msimu mmoja hadi mwingine ndani au nje ya mbegu, kwenye udongo na pia kwenye mabaki ya mimea iliyoambukizwa. Huenea kupitia maji, mvua, upepo na mguso wa majani hadi majani na kwenye zana, na wafanyakazi. Maambukizi ya majani hutokea kwa kupenya moja kwa moja kwenye jani na hupendezwa na unyevu wa muda mrefu wa majani. Hali bora ya kuambukizwa ni joto la 23 ° C na unyevu wa 77-85%. Ikiwa hali hizi zitatimizwa, kuna uwezekano mkubwa wa kuathiri mavuno kwa kiasi kikubwa, hasa ikiwa maambukizi hutokea mwanzoni mwa msimu.


Hatua za Kuzuia

  • Hakikisha unapata mbegu zenye afya, zilizothibitishwa.
  • Weka nafasi kati ya mimea kama inavyo shauriwa ili kuruhusu mzunguko mzuri wa hewa na kuepuka muda mrefu wa unyevu wa majani.
  • Tumia matandazo kuunda kizuizi kati ya mmea na kuvu.
  • Tumia vigingi kuweka mimea wima.
  • Tumia mfumo wa umwagiliaji kwa njia ya matone ili kupunguza unyevu kwenye majani.
  • Fuatilia vitalu vya mbegu, mimea michanga au vipandikizi kwa dalili zozote za ugonjwa.
  • Ondoa mimea iliyoambukizwa na uiharibu mbali na shamba.
  • Dhibiti magugu yanayohifadhi kuvu ndani na nje ya shamba.
  • Usifanye kazi kwenye shamba wakati mimea ina unyevu.
  • Tekeleza mzunguko mpana wa mazao, angalau kwa kipindi cha miaka 3.
  • Ondoa uchafu wa mimea baada ya kuvuna na kuharibu.
  • Hakikisha matunda yaliyochaguliwa kwa ajili ya mbegu hayana muoza wa shina.

Pakua Plantix