Mtama

Chule ya Baka-jani na Muozo wa Shina

Colletotrichum graminicola

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Vidonda vidogo, vya mviringo, vilivyo na maji kwenye majani.
  • Madoa yenye vitovu vya kahawia na kingo za zambarau.
  • Maabaka ya viraka hufunika jani zima.
  • Mmea kufa kuanzia juu kurudi chini.
  • Kuoza kwa shina.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Mtama

Dalili

Aina ya mmea, hali ya mazingira na nguvu ya vimelea huamua matokeo ya maambukizi. Kwa aina zinazoshambuliwa, maambukizi yana sifa ya awamu tatu tofauti: mabaka ya majani, mmea kufa kuanzia juu, na kuoza kwa shina. Vidonda vidogo vya mviringo, vilivyojaa maji huonekana kwanza kwenye majani ya chini, karibu na ncha ya jani au kwenye mshipa mkuu wa katikati, na baadaye kwenye sehemu ya juu. Huongezeka na kuwa madoa yanayo angaza kiasi yenye vitovu vya hudhurungi na kingo za rangi ya zambarau na huweza kuungana na kutengeneza viraka vyenye mabaka ambayo hufunika jani zima (Baka la majani). Katika hatua za baadaye za ukuaji wa mmea, alama zenye weusi, zilizoinuliwa huonekana kwenye tishu zilizokufa ikiwa hali ni rafiki. Majeraha ya mabua na mashina yanapelekea kutawaliwa kwa tishu za ndani ambazo husababisha dalili zingine kama vile kufa kuanzia juu na kuoza kwa bua.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hatujui matibabu yoyote bora dhidi ya Colletotrichum graminicola. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa unajua chochote kinachoweza kusaidia kupambana na ugonjwa huu. Tunatarajia kusikia kutoka kwako.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Hadi sasa, hakuna dawa za kuvu zenye ufanisi zinazopatikana.

Ni nini kilisababisha?

Kuvu huishi katika mabaki ya mimea kwenye udongo, kutokea hapo husambazwa kwenye majani ya chini na upepo na mvua inayonyesha wakati wa majira ya kuchipua. Vidonda vinavyotokea kwenye bapa za majani husababisha kuenea kwa upili kwenye majani ya juu au mabua. Majeraha ya shina huongeza uwezekano wa kutawaliwa kwa tishu za ndani. Ikiwa hali ya mazingira ni nzuri, dalili zingine kama vile kufa kuanzia juu na kuoza kwa bua huonekana. Mzunguko wa maisha ya Kuvu (na ugonjwa) hupendelewe na halijoto ya joto kiasi (20 hadi 30°C), unyevu wa hali ya juu kwa kipindi kirefu, na mvua ya mara kwa mara. Kuvu anaweza kuambukiza mimea katika hatua ya miche lakini mara chache husababisha hasara kubwa ya mavuno ikiwa shamba limerutubishwa ipasavyo. Majani yanayokua kwa haraka hayana uwezekano wa kupata dalili.


Hatua za Kuzuia

  • Panda aina sugu kama zinapatikana katika soko lako.
  • Panga mzunguko wa mazao wa muda mrefu na mazao yasiyo shambuliwa (mazao yasiyo ya nyasi au soya).
  • Fuatilia shamba kwa uwepo wa dalili, kwa mfano kuoza kwa shina.
  • Dumisha rutuba ya udongo iliyosawia na viwango thabiti vya pH.
  • Mashamba yawe na mfumo wa kupitisha maji vizuri.
  • Dhibiti magugu ndani na nje ya shamba.
  • Lima kwa kina baada ya kuvuna na uzike mabaki.

Pakua Plantix