Nothophoma arachidis-hypogaeae
Kuvu
Vidonda vya duara hadi visivyo na umbo maalumu vyenye rangi ya hudhurungi nyepesi vilivyo zungukwa na kingo za rangi ya kahawia nyekundu huonekana kwenye majani. Ugonjwa unapoendelea, katikati ya kidonda huwa kijivu na kukauka, katika baadhi ya matukio hatimaye sehemu hizo hupolomoka, na kuacha tundu na kuyapa majani muonekano wa kuchanika. Vidonda vinaweza kuungana na kuunda mabaka makubwa, yasiyo na umbo maalumu, yenye tishu zilizo kufa. Madoa meusi yanayofanana na pilipili huonekana ndani ya tishu zilizo na ugonjwa kwenye nyuso zote za majani.
Samahani, hatujui matibabu yoyote mbadala dhidi ya ugonjwa huu wa fangasi. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa unajua kitu ambacho kinaweza kusaidia kupambana na ugonjwa huu. Tunatarajia kusikia kutoka kwako.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Uharibifu kutokana na Doajani la Phyllosticta kwa kawaida ni mdogo, kwa hiyo dawa za kuua kuvu hazipendekezwi sana.
Kuvu anaweza kubaki hai kwa takriban mwaka mmoja katika uchafu wa mazao ulioambukizwa kwenye udongo. Kutoka kwenye udongo, kwa kawaida huambukiza tishu zilizoharibiwa na zilizo kufa za mimea iliyoathiriwa na magonjwa mengine au kujeruhiwa wakati wa kazi za shambani (maambukizi ya upili). Kisha huenea kwa tishu zenye afya na husababisha dalili maalum. Hali bora kwa ukuaji wa kuvu na ukuaji wa ugonjwa ni joto kati ya 25-30 ° C na pH kati ya 5.5-6.5. Doajani Phyllosticta halichukuliwi kama ugonjwa mkubwa wa karanga.