Botrytis cinerea
Kuvu
Ukuaji mkubwa wa ukungu kwenye majani, vikonyo, maganda au matunda ndio dalili inayo shambulia zaidi. Mwanzoni, vidonda vilivyotawanyika, vya hudhurungi na vilivyotota maji huonekana kwenye sehemu za mmea ambazo zimegusana na ardhi au zilizojeruhiwa. Viraka vingi vyenye manyoya na rangi ya kijivu-kahawia vya ukuaji wa kuvu hutokea kwenye tishu hizi. Baadaye, ukungu hukua kwenye matunda machanga na maganda madogo, na kuyapa mwonekano wa sufi. Vinginevyo, dalili huonekana wakati wa kuhifadhi. Katika visa vyote viwili, hasara kubwa inaweza kutarajiwa. Kuoza kwa majani ya chini na shina husababisha kukosekana kabisa kwa mazao hasa katika aina za mazao ya bustani ambazo ni nyepesi kushambuliwa (kinyausi). Mara chache, kufa kwa matawi na uwepo wa vikwachu kumeonekana kwenye mazao ya miti.
Dawa za kuua kuvu za asili zenye kuvu washindani waitwao Trichoderma harzianum ni nzuri dhidi ya ukungu wa kijivu kwenye mazao mbalimbali. Bidhaa zenye Streptomyces griseovirides pia zinapatikana kwa matumizi kwenye mboga aina ya letusi.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia na matibabu ya kibayolojia, ikiwa yanapatikana. Udhibiti ni mgumu kufanikiwa kwa sababu kuvu anaweza kutawala mimea mwenyeji karibu na wakati wa kuvuna, na hivyo kuzuia uwekaji wa kemikali zinazoacha mabaki ya sumu. Katika hali ya maambukizi ya mapema, dawa ya kupuliza ya majani yenye chlorothalonil inaweza kutumika kudhibiti kuenea kwake. Dawa zingine za kuvu zenye fluazinam, na thiophante-methyl pia zinaweza kufanya kazi. Maendeleo ya ukinzani ni ya kawaida endapo dawa za kuua kuvu zitatumiwa kwa kiasi kikubwa.
Dalili husababishwa na fangasi anae enea kwa njia ya udongo aitwae Botrytis cinerea ambae huweza kukua na kuambukiza sehemu zote za mmea. Hali ya hewa ya unyevu, na mvua ya mara kwa mara na joto la wastani hupelekea kuonekana kwa dalili. Kiwango bora cha joto kilichoripotiwa kwa ukuaji wa Kuvu, ushambuliaji wa mmea na maendeleo ya ugonjwa ni 15-20 ° C. Dalili huonekana kwanza kwenye majani au sehemu za mimea ambazo zimejeruhiwa na mitambo wakati wa kazi za shambani au kupitia mvua ya mawe au barafu. Majani ya chini yana hatari zaidi. Umwagiliaji kupita kiasi na kivuli kikubwa kinaweza kuongeza kiwango cha ugonjwa kwa kuweka mazingira yenye unyevunyevu na mnene ambayo ni rafiki kwa ukuaji wa kuvu.