Rhizoctonia solani
Kuvu
Dalili za awali za ugonjwa huo ni vidonda kwenye mashina (vifuko-jani) karibu na mstari wa maji. Vidonda hivi ni vya mviringo, kijivu-kijani, urefu wa 1-3 cm na vimetota a maji. Vidonda hivi hukua bila mpangilio na kugeuka kijivu hadi vyeupe na kingo za kahawia. Ugonjwa unapoendelea, sehemu za juu za mmea huambukizwa. Kwenye sehemu hizi, vidonda vinavyo kua kwa kasi huonekana na jani zima hubabuka. Hii inaweza kusababisha kifo cha jani na mmea mzima. Zaidi ya hayo, malengelenge ya kuvu huundwa kwenye uso wa mmea.
Kwa bahati mbaya, hakuna mbinu bora za udhibiti wa kibiolojia zinazopatikana kwa wakati huu.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Ili kuzuia maambukizi, tumia dawa za kuua kuvu zifuatazo: hexaconazole 5EC (2 ml/l) au validamycin 3L (2ml/l) au propiconazole 25 EC (1ml/l) au trifloxystrobin + tebuconazole (0.4g/l). Badilisha dawa mara mbili kwa muda wa siku 15.
Hali zinazofaa kwa ugonjwa wa Baka la Kifuko-jani cha Mpunga ni joto la juu kati ya 28 na 32°C, viwango vya juu vya mbolea ya naitrojeni na unyevu wa juu wa 85-100%. Hasa wakati wa mvua, hatari ya kuambukizwa na kuenea kwa ugonjwa huu ni kubwa. Dari ya mimea iliyo funga huchochea hali ya unyevunyevu na mgusano. Kuvu huishi kwenye udongo kwa miaka kadhaa kama sclerotium iliyolala/bwete. Huelea juu wakati mashamba yakijaa mafuriko. Mara baada ya kugusana na mmea wa mpunga, kuvu huingia kwenye kifuko-jani/ala ya jani, kuanza mchakato wa maambukizi.