Ndizi

Ugonjwa wa Panama

Fusarium oxysporum

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Majani ya zamani/yaliyokomaa hugeuka kuwa ya njano na kunyauka.
  • Majani yanageuka kuwa ya kahawia na kudondoka.
  • Shina kupasuka.
  • Michirizi ya manjano hadi myekundu kwenye mashina.
  • Kubadilika kwa rangi ya tishu za ndani.
  • Sehemu zote za mmea hatimaye huoza na kufa.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Ndizi

Dalili

Dalili zinaweza kutofautiana kidogo kutegemea na aina ya migomba, nguvu ya vimelea vya magonjwa na hali ya mazingira. Ugonjwa huathiri majani ya zamani/makuu kuu kwanza na hatua kwa hatua huenda juu hadi kwa majani machanga. Sifa za ugonjwa huo ni majani ya manjano na yaliyokauka na vikonyo na kupasuka kwa kitako cha shina. Majani yenye ugonjwa yanageuka kuwa ya kahawia, makavu na hatimaye kuanguka kwenye kikonyo, na kutengeneza kitu mithili ya sketi kuzunguka shina. Michirizi ya njano hadi myekundu inaonekana kwenye shina, inakuwa mikali zaidi kwenye kitako. Sehemu ya ndani ya tishu zinaonyesha kubadilika rangi kutoka nyekundu hadi kahawia, dalili ya ukuaji wa fangasi na kuoza kwa tishu. Hatimaye, sehemu zote za juu na chini ya ardhi huoza na kufa.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Utumiaji wa viumbe wa udhibiti wa kibaiyolojia kama vile fangasi aina ya Trichoderma viride au bakteria aitwae Pseudomonas fluorescens kwenye udongo ni mbinu bora za kupunguza matukio na ukali wa ugonjwa.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Kinyume na magonjwa mengine ya fangasi/kuvu katika mnyauko fusari wa migomba, mara unapogunduliwa, hauwezi kudhibitiwa na dawa za kuua kuvu/ukungu. Kuzamisha vichipukizi kwenye dawa maalum za kuua ukungu (10g/10 lita za maji) ikifuatiwa na kumwagilia udongo majimaji yenye dawa kila mwezi wa pili kuanzia miezi 6 baada ya kupanda inapendekezwa.

Ni nini kilisababisha?

Ugonjwa wa Panama (pia huitwa Mnyauko Fusari Wa Migomba) husababishwa na spishi ndogo ya Kuvu aitwae Fusarium oxyporum, ambae anaweza kuishi kwenye udongo kwa miongo kadhaa. Kuvu hawa huingia kwenye mmea kwa njia ya nywele ndogo za mizizi, mchakato ambao unaorahisishika zaidi katika udongo mwepesi, usiopitisha maji vizuri. Kuvu husambazwa umbali mfupi na maji yaliyo juu ya ardhi, vyombo vya moto (magari, n.k), zana na viatu. Nyenzo za upandaji zilizoambukizwa, kwa upande wake, ndiyo njia ya kawaida ya kueneza ugonjwa kwa umbali mrefu. Joto la juu ni sehemu muhimu katika maendeleo ya ugonjwa huo. Majani kugeuka manjano na ukosefu wa uimara wa mimea hutokana na kuoza kwa tishu zinazosafirisha chakula na maji katika shina. Ikiwa hali zote zitatimizwa, Mnyauko Fusari unaweza kuwa ugonjwa hatari sana katika ndizi.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia nyenzo za upandaji zenye afya tu kutoka kwa vyanzo vilivyoidhinishwa.
  • Panda aina za mimea ambazo ni sugu dhidi ya magonjwa na wadudu ikiwa inapatikana.
  • Hakikisha kuna mfumo mzuri wa kupitisha maji.
  • Kagua mimea kila baada ya wiki ya pili.
  • Tumia dawa za kuua magugu ili kuua mimea yenye magonjwa.
  • Ng'oa mimea iliyoathiriwa sana na ichome moto mara moja.
  • Jihadhari na kusafirisha udongo bila kukusudia kutoka maeneo yaliyoambukizwa hadi maeneo safi.
  • Takasa zana, vifaa na mashine za kilimo kwa kutumia jiki ya sodium hypochlorite.
  • Usipande migomba kwenye udongo ulioathirika sana kwa miaka 3-4 ijayo.
  • Fanya kilimo cha mzunguko kwa kuzungusha na miwa, mpunga au alizeti ili kupunguza matukio ya magonjwa.
  • Mseto na vitunguu vya Kichina (Allium tuberosum).
  • Kuza uwepo wa viumbe wadogo ambao wanazuia ukuaji wa Kuvu.

Pakua Plantix