Ndizi

Chule ya Ndizi

Colletotrichum musae

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa ya kahawia-nyeusi hadi nyeusi, yaliyozama kwenye matunda.
  • Hukua na kuwa madoa/viraka vikubwa.
  • Ukuaji wa kuvu wenye rangi ya chungwa hadi lax katikati mwao.
  • Kuiva kabla ya kukomaa na kuoza.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Ndizi

Dalili

Kuvu husababisha madoa ya kahawia-nyeusi hadi nyeusi kamili, yaliyozama kwenye ganda la matunda yaliyoambukizwa. Dalili za awali zinaonekana kwenye matunda ya kijani, na zina sifa ya kuwa na rangi yenye weusi wa kahawia hadi dengu nyeusi, vidonda vilivyozama vyenye ukingo wa rangi iliyopauka kwenye ganda. Kwenye matunda ya manjano, vidonda hivi vinakuwa na ukubwa tofauti na vinaweza kuungana na kuwa mabaka meusi yaliyozama. Ukuaji wa kuvu wenye rangi ya machungwa hadi waridi (pinki) huonekana katikati ya matunda. Dalili zinaweza pia kuanza kuonekana kwenye ncha ya matunda na kusababisha maambukizi ya zamani ya maua. Matunda yaliyoathiriwa yanaweza kuiva kabla ya wakati, na nyama ya tunda kuendelea kuathiriwa na kuoza. Dalili za kwanza zinaweza pia kuonekana muda mrefu baada ya kuvuna, wakati wa usafiri au kuhifadhi.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Matibabu ya matunda wakati wa kuvuna kwa kutumia dawa za kuua kuvu zinazotokana na 10% ya ubani pamoja na 1.0% ya chitosan (inayotokana na chitin) imethibitishwa kudhibiti ugonjwa huo wakati wa kuhifadhi. Aina mbalimbali za mchanganyiko wa mimea zimetumika kwa mafanikio fulani ili kuzuia ukuaji wa vimelea vya ugonjwa huo, ikiwa ni pamoja na vizidio (extract) vya jamii ya machungwa, viziduo vya tangawizi pamoja na viziduo vya majani za Akasia nyeupe, Polyalthia longifolia na Clerodendrum inerme. Data hizi zinazoleta matumaini bado zinahitaji kuthibitishwa katika majaribio ya shambani. Kuzamishwa kwa matunda ya kijani katika maji ya moto yenye nyuzi 55 ° C kwa dakika 2 pia hupunguza athari za ugonjwa huu.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Wakati wa kilimo, mikungu ya migomba inaweza kunyunyiziwa kwa bidhaa zenye mancozeb (0.25%) au benzimidazole (0.05%) na baadaye kufunikwa ili kuzuia uchafuzi wowote. Matunda yaliyovunwa yanaweza kuchovywa au kunyunyuziwa dawa za kuua ukungu zenye benzimidazole. Kupaka matunda kwa kemikali zinazotumika kuhifadhi vyakula kama vile butylated hydroxyanisole (BHA) kunaweza kuwa na uwezo wa kuboresha ufanyaji kazi wa dawa hizi za kuua ukungu.

Ni nini kilisababisha?

Chule au kuvu husababishwa na fangasi anayeitwa Colletotrichum musae, ambao huishi kwenye majani yaliyokufa au kuoza na pia kwenye matunda. Vijimbegu vyake vinaweza kuenezwa na upepo, maji na wadudu pamoja na ndege na panya wanaokula ndizi. Fangasi au kuvu hawa wanaingia kwenye tunda kupitia majeraha madogo kwenye maganda na baadaye huota na kuanzisha udhihirisho wa dalili. Hali nzuri ya mazingira kwa maambukizi kutokea ni joto la juu, unyevu wa juu na mvua za mara kwa mara. Dalili zinaweza kutokea wakati matunda yanayoiva kwenye vicha au vishada vya miti au baada ya kuvuna wakati wa kuhifadhi. Ni ugonjwa mkuu unaoathiri ubora wa matunda ya ndizi wakati wa usafirishaji na kuhifadhi.


Hatua za Kuzuia

  • Epuka uharibifu wa tishu za ndizi wakati wa kuvuna, kufungasha na kuhifadhi.
  • Tumia mifuko ya plastiki baada ya mikungu kuibuka ili kuilinda mikungu dhidi ya uchafu.
  • Safisha vituo vya kusindika na kuhifadhi ili kuzuia uchafuzi wa baada ya kuvuna.
  • Osha matunda kwa maji ili kuondoa ngozi kutoka kwenye vijimbegu vya kuvu.
  • Ondoa majani yaliyooza na sehemu zilizobaki za maua.

Pakua Plantix