Trachysphaera fructigena
Kuvu
Tabia za ugonjwa ni uwepo wa uozo mkavu, wenye rangi ya kijivu hadi nyeusi kwenye ncha za ndizi. Ukuaji wa kuvu hasa huanza katika hatua ya utokaji wa maua na hivyo kuhatarisha mchakato wa kuiva kwa matunda. Maeneo yaliyoathiriwa yanafunikwa na ukuaji wa ukungu wa rangi ya kijivu ambao huonekana kama majivu kwenye ncha ya sigara iliyochomwa/inayovutwa, na hivyo kupata jina la ugonjwa huo. Katika kuhifadhi au wakati wa usafiri ugonjwa unaweza kuendelea kuhusisha tunda zima, na kusababisha mchakato wa ukaukaji kama maiti. Matunda yana umbo lisilo la kawaida, ukungu (fangasi) huonekana dhahiri kwenye matunda na vidonda vinaonekana wazi kwenye ngozi.
Dawa za kupuliza zinazotokana na magadi ya kuokea zinaweza kutumika kudhibiti Kuvu. Ili kutengeneza dawa hii, yeyusha gramu 100 za magadi ya kuokea na gramu 50 za sabuni kwenye lita 2 za maji. Nyunyiza mchanganyiko huu kwenye matawi yaliyoambukizwa na kwenye matawi ya karibu ili kuzuia maambukizi. Hii huongeza viwango vya tindikali na alkali, yaani pH ya chane za ndizi na huzuia ukuaji wa Kuvu. Vinyunyuzi vya viua kuvu vya shaba vinaweza kufaa vile vile.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Kwa kawaida ugonjwa huu una umuhimu mdogo na mara chache uhitaji udhibiti wa kwa kutumia madawa ya kikemekali. Mikungu iliyoathirika inaweza kunyunyiziwa na mancozeb, triophanate methyl au metalaxyl mara moja na baadae kufunikwa na mifuko ya plastiki.
Majivu Nchani mwa Matunda ni ugonjwa wa ndizi unaosababishwa hasa na fangasi/kuvu anayefahamika kama Trachysphaera fructigena na wakati mwingine fangasi mwingine (Verticillium theobromae). Ugonjwa huu husafirishwa kwa njia ya upepo au mvua hadi kwenye tishu zenye afya. Kuvu hushambulia migomba katika hatua ya utokaji wa maua wakati wa msimu wa mvua. Huambukiza ndizi kupitia maua. Kutoka hapo, baadaye huenea kwenye ncha ya tunda na husababisha muozo mkavu ambao ni sawa na majivu ya sigara, na hivyo kupatikana kwa jina lake la kawaida. Maambukizi ni ya kawaida katika siku za mwanzo baada ya kuibuka kwa matunda na katika hali ya joto la unyevu, hasa katika maeneo ya mwinuko wa juu na katika mashamba yaliyo katika maeneo ya kivuli.