Oidium caricae-papayae
Kuvu
Madoa yenye maji maji yaliyo funikwa na jamvi la kuvu wa unga mweupe huonekana kwanza kwenye sehemu ya chini ya majani, mara nyingi karibu na mishipa ya majani, kwenye vikonyo vya majani na chini ya maua. Wakati mwingine, madoa ya rangi ya kijani mpauko au njano hutokea upande wa juu wa majani, wakati mwingine hufunikwa na ukungu mweupe. Madoa haya yanaweza kugeuka kahawia yenye seli zilizokufa yakizungukwa na upinde wa njano baadaye. Majani yaliyo athirika zaidi baadaye hujikunja kueleke ndani. Matunda yanaweza kuonyesha kama jamvi la ukungu mweupe kwa kiasi tofauti. Maambukizi kwa ujumla husababisha uharibifu mdogo kwa miti yenye umri mkubwa inayozaa. Hata hivyo, katika mimea michanga huweza kusababisha kufa kwa tishu zinazoongezeka, majani kuanguka, vidonda vya shina na matunda na hasara kubwa kwenye mavuno.
Salfa yenye unyevunyevu, vumbi la salfa, au salfa ya chokaa pamoja na bikarboneti ya potasiamu vimeonekana kusaidia katika kudhibiti ugonjwa huu. Hata hivyo, matibabu haya yanaweza kuwa na sumu kwa mimea ikiwa hutumiwa wakati wa joto. Katika baadhi ya matukio, poda ya kuokea mikate, mafuta ya mwarobaini na kimiminika cha sabuni inaweza kufaa. Kwa ujumla, matibabu haya hayafai endapo ugonjwa huo ni mkali.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa inapatikana. Dawa za kuua kuvu kama vile azoxystrobin, mancozeb zinaweza kutumika kudhibiti ubwiri unga kwenye papai.
Ugonjwa huu husababishwa na kuvu/fangasi aina ya Oidium caricae-papayae. Kuvu hawa huishi na kuzaliana kwenye mimea ya mipapai pekee. Chavua za kuvu hutawanywa kutoka kwa mmea hadi mmea na kati ya shamba kwa upepo. Majani katika hatua zote za ukuaji yanaweza kuathiriwa, lakini majani yaliyokomaa huathirika zaidi. Kuvu hutawala seli za juu kwenye ngozi ya mmea, ndicho husababisha dalili kuonekana. Maendeleo ya ugonjwa huo na ukali wa dalili hukuzwa na viwango vya chini vya mwanga, kiwango cha juu cha unyevu, joto la wastani (18 hadi 32 ° C), na mvua kutoka 1500 hadi 2500 mm kwa mwaka