Cercospora canescens
Kuvu
Dalili hutofautiana kidogo kutegemeana na nguvu ya vimelea na aina ya mmea. Madoa madogo ya duara na yenye maji yakiwa na rangi ya kahawia katikati na duara la mwanga wa njano hutokea kwanza kwenye majani wiki ya 3-5 baada ya kupanda zao. Katika hatua za baadaye za ugonjwa, madoa huongezeka na kuwa na rangi ya kahawia (kutokana na kufa kwa tishu za majani), kingo zenye rangi ya kahawia iliyochanganyika na wekundu ambazo zinaonekana zimebonyea kidogo. Madoa haya yanaweza pia kutokea kwenye sehemu zote za mmea, hususani kwenye maganda mabichi. Katika mazingira muafaka kwa ugonjwa huu, madoa mengi kwenye majani yanaweza kusababisha majani kupukutika kwa wingi wakati wa kutoa maua na utengenezaji maganda. Kuvu (ukungu) hukua juu na ndani ya maganda, na kuyaharibu kabisa, na mara nyingi kusababisha upotevu wa mavuno kwa asilimia 100.
Matibabu ya mbegu kwa kutumia maji ya moto yanawezekana. Matumizi ya mafuta ya mwarobaini pia yana ufanisi katika kupunguza makali ya ugonjwa (idadi kubwa ya maganda na mbegu, maganda yenye afya, na uzito wa juu).
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kinga pamoja na tiba za kibailojia ikiwa zinapatikana. Ikiwa matibabu kwa kutumia dawa za kuua kuvu/ukungu yanahitajika, tumia dawa zenye mancozeb, chlorothalonil kwa kipimo cha 1g/l, au thiophenate methyl kwa kipimo cha 1 ml mara mbili kwa kila baada ya siku 10.
Ugonjwa wa madoa kwenye majani unasababishwa na kuvu anayefahamika kitaalamu kama Cercospora canescens, ambae huambukiza choroko nyeusi na za kijani. Kuvu huyu husambazwa kwa njia ya mbegu na anaweza kuishi kwa zaidi ya miaka miwili kwenye mabaki ya mimea yaliyoko ardhini. Kupitia mfumo wa mizizi, kuvu wanaweza kusafiri kwa umbali mrefu ndani ya udongo. Kuvu hawa pia hustawi kwenye mimea mbadala inayoweza kuhifadhi vimelea au kwenye mazao yanayoota yenyewe shambani. Usambaaji wa kuvu hadi sehemu za chini za mmea hutokea kupitia rasharasha za maji na hewa. Hali ya joto la juu wakati wa mchana na usiku, udongo wenye unyevu, unyevu mwingi wa anga, au mvua kubwa; yote hayo yanatengeneza mazingira muafaka ya kusambaza kuvu.