Mahindi

Baka Jani la Kaskazini

Setosphaeria turcica

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Dalili huonekana kwanza kwenye majani ya chini, yakiwa na vidonda virefu na vyembamba vya rangi ya kahawia sambamba na kingo za majani zenye urefu wa milimita 25-150.
  • Ugonjwa huu husababisha majani kukauka, kuharibika na kufa.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Mahindi

Dalili

Dalili huonekana kwanza kama madoa madogo kwenye majani ya chini, yakiwa na umbo la yai na yaliyotota maji. Kadri ugonjwa unavyoendelea, yanaanza kuonekana kwenye sehemu ya juu ya mmea. Madoa ya zamani polepole yanakua na kugeuka vidonda vinavyotokana na kufa kwa tishu, huku vikiwa na umbo refu la sigara na madoa ya wazi yenye rangi ya Giza na kingo za kijani iliyopauka ambazo zimetota maji. Madoa haya baadaye huungana na kufunika sehemu kubwa ya jani na shina, wakati mwingine yakisababisha kifo cha mmea na kuanguka. Ikiwa maambukizi yanasambaa hadi sehemu za juu za mmea wakati wa ukuaji wa mabunzi/magunzi, hasara kubwa ya mavuno inaweza kutokea (hadi asilimia 70%).

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Dawa za kibaiolojia za kuua/kuudhibiti kuvu zinazotokana na Trichoderma harzianum au Bacillus subtilis zinaweza kutumika katika hatua mbalimbali ili kupunguza hatari ya maambukizi. Matumizi ya mchanganyiko la salfa pia yana ufanisi.

Udhibiti wa Kemikali

Inapendekezwa matumizi ya mbinu jumuishi zenye hatua za kinga pamoja na kutumia kwa uangalifu mbinu za asili za kuudhibiti magonjwa. Matumizi ya Mapema ya dawa za kuua kuvu kama hatua ya kinga yanaweza kuwa njia bora ya kudhibiti ugonjwa. Vinginevyo, dawa za kuua kuvu zinaweza kutumika wakati dalili zinapoonekana kwenye majani ya chini ili kulinda majani ya juu na masuke. Pulizia dawa zinazotokana na azoxystrobin, picoxystrobin, mancozeb, pyraclostrobin, propiconazole, na tetraconazole. Tumia bidhaa za dawa zinazotokana na picoxystrobin + cyproconazole, pyraclostrobin + metconazole, propiconazole + azoxystrobin, na prothioconazole + trifloxystrobin. Matibabu ya mbegu hayapendekezwi.

Ni nini kilisababisha?

Kuvu huishi kwenye udongo au kwenye mabaki ya mimea wakati wa msimu wote wa baridi. Mvua, umande wa usiku, unyevu wa kiwango cha juu, na joto la wastani, yote hayo yanasaidia kusambaa kwa kuvu. Wakibebwa na kusambazwa na upepo au matone ya mvua, huanza kuenea kutoka kwenye udongo hadi kwenye majani ya chini ya mimea michanga ya mahindi. Hali za mvua na mbinu mbaya za kilimo huchangia kuenea kwa kuvu kutoka mmea mmoja hadi mwingine na ndani ya shamba hilo hilo. Kiwango muafaka cha joto kuwezesha maambukizi ni kati ya nyuzijoto 18 hadi 27°C wakati wa msimu wa ukuaji. Kipindi kirefu cha saa 6 hadi 18 cha maji maji kwenye majani pia ni muhimu kwa ukuaji wa kuvu. Mtama ni zao lingine mbadala linalopendwa na kuvu huyu kuishi.


Hatua za Kuzuia

  • Panda aina ya mbegu zenye ukinzani au zinazostahimili ugonjwa.
  • Hakikisha kunakuwa na uwiano sahihi wa virutubisho vya udondo na epuka matumizi ya mbolea ya naitrojeni kwa wingi.
  • Mara kwa mara ondoa magugu yaliyopo shambani na yanayozunguka shamba.
  • Fanya kilimo cha mzunguko wa mazao kwa kupokeza na soya, maharagwe, au alizeti ili kuepusha kuenea ugonjwa kwa kiasi kikubwa.
  • Lima kwa kwenda chini zaidi ili kuyazika mabaki ya mimea na kupunguza kiwango cha virusi katika udongo.

Pakua Plantix