Mpunga

Baka Kahawia la Mpunga

Cochliobolus miyabeanus

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Mabaka ya mviringo yenye rangi ya kahawia kwenye majani machanga.
  • Kingo zenye wekundu kwenye mimea iliyokomaa.
  • Shina na majani huwa na rangi ya njano na kunyauka.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Mpunga

Dalili

Ugonjwa huu una sifa ya kuwa na dalili mbalimbali. Hata hivyo, uwepo wa mabaka ya mviringo au ya umbo la yai, yenye duara la rangi ya manjano yakiwa na umri mkubwa ni ishara inayoonekana zaidi ya maambukizi. Kadri yanavyo kua, mabaka hayo huwa na rangi ya kijivu katikati na kuzungukwa na ukingo wa rangi ya kahawia inayokaribia nyekundu. Shina pia hubadilika rangi. Kwa aina za mbegu zisizo na ukinzani, mabaka/vidonda vinaweza kufikia urefu wa 5-14 mm na kusababisha majani kunyauka. Kwa aina za mbegu zinazostahimili, mabaka/vidonda vina rangi ya njano inayokaribia kahawia na ukubwa wa kichwa cha sindano. Maambukizi katika masuke husababisha kupungua kwa idadi ya punje kwenye suke na kupungua kwa ubora wa punje.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Ili kuhakikisha kuwa mbegu hazina vimelea vya magonjwa, unashauriwa kuloweka mbegu katika maji ya moto (53-54 ° C) kwa dakika 10 hadi 12. Ili kuboresha matokeo, weka mbegu kwa saa 8 kwenye maji baridi kabla ya kuloweka kwenye maji ya moto.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi yenye hatua za kinga na matibabu ya kibayolojia ikiwa inapatikana. Njia bora ya kuzuia ugonjwa huo ni kutumia dawa za kuua kuvu (kwa mfano, iprodione, propiconazole, azoxystrobin, trifloxystrobin) kama matibabu ya mbegu

Ni nini kilisababisha?

Ugonjwa huu husababishwa na kuvu/fangasi anaejulikana kama Cochliobolus miyabeanus. Kuvu huyu anaweza kuishi kwenye mbegu kwa zaidi ya miaka minne na kuenea kutoka kwa mmea hadi mmea kupitia chavua zinazopeperuka hewani. Mabaki ya mimea iliyoambukizwa iliyoachwa shambani na magugu ni njia nyinginezo za kawaida za kueneza ugonjwa huo. Madoa/mabaka ya kahawia yanaweza kutokea katika hatua zote za mmea, lakini maambukizi huwa ya juu zaidi wakati wa mmea kuchanua hadi hatua ya kukomaa. Ugonjwa huu mara nyingi hutokea katika mashamba yenye usimamizi mbaya wa rutuba ya udongo, hasa katika suala la virutubisho vinavyohitajika kwa kiasi kidogo na mmea (micronutrients). Udhibiti mkubwa wa Baka kahawia la mpunga umefanikiwa kwa kutumia mbolea zenye silikoni. Matumizi ya mchanganyiko wa samadi ya ng'ombe na mbolea za kemikali kwa kiasi fulani pia hupunguza makali ya ugonjwa huu. Unyevu mwingi (86-100%), unyevu wa muda mrefu wa majani na joto la juu (16-36 ° C) ni mazingira rafiki sana kwa kuvu/fungasi wa ugonjwa wa Baka Kahawia la mpunga.


Hatua za Kuzuia

  • Kwa udongo wenye kiasi cha chini cha madini ya silikoni, tumia slagi ya siliketi ya kalisi (calcium silicate slag) kabla ya kupanda.
  • Tumia aina ya mbegu zenye zinazohimili magonjwa ikiwa zinapatikana.
  • Pata mbegu zako kutoka kwenye vyanzo vilivyoidhinishwa ikiwezekana.
  • Hakikisha ugavi wa virutubishi sawia na ufuatilie kiasi cha virutubisho katika udongo mara kwa mara.
  • Fuatilia mashamba yako kujua kama kuna dalili za ugonjwa kuanzia hatua ya kulima.
  • Dhibiti na uondoe magugu ndani na nje ya shamba lako.
  • Ondoa na uharibu mimea iliyoambukizwa, kwa kuichoma baada ya mavuno.

Pakua Plantix