Muwa

Fugwe ya Miwa

Sporisorium scitamineum

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Muonekano unaofanana na mjeledi mweusi hukua kwenye mmea.
  • Kudumaa kwa ukuaji wa mmea.
  • Majani membamba yaliyokakamaa (magumu).

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Muwa

Dalili

Kitu cheusi, chembamba chenye mwonekano kama mjeledi hutokeza kwenye sehemu ya muwa na kukua. Kitu hicho kawaida hujitokeza sehemu ya juu ya mmea ulioathiriwa. Huundwa kwa mchanganyiko wa tishu za miwa na tishu za kuvu. Chavua/vijimbegu vya Kuvu huhifadhiwa ndani ya hicho kitu chenye umbo kama mjeledi. Mara baada ya chavua kutolewa, sehemu ya katikati ya tu ya huo mjeledi hubakia. Mmea wa miwa pia huacha kukua na majani yake kuwa membamba na magumu.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Ondoa mabua yaliyoambukizwa na haribu mabaki yote ya mimea iliyoambukizwa. Ili kuhakikisha mbegu zisizo na magonjwa, tumbukiza vipandikizi vya miwa katika maji moto ya 52°C kwa dakika 30.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi yenye hatua za kinga pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Matibabu ya seti kwa dawa za kuua kuvu kama vile benzimidazole kabla ya kupanda inaweza kusaidia kupunguza matukio ya ugonjwa mashambani.

Ni nini kilisababisha?

Chavua/Vijimbegu vya ugonjwa vinavyotoka kwenye kitu chenye muundo kama mjeledi huenezwa na upepo na wadudu. Pia vinaweza kusambazwa wakati watu wakitumia vipandikizi ya miwa iliyoambukizwa kuanzisha mimea mipya. Ugonjwa huo una uwezekano mkubwa wa kuenea wakati wa joto na unyevu. Mimea iliyoambukizwa inaweza kukua kwa miezi kadhaa bila kuonyesha dalili zozote za ugonjwa. Baada ya miezi miwili hadi minne (wakati fulani hadi mwaka mmoja), sehemu ya juu ya miwa inayokua huanza kutoa kitu chenye muundo unaofanana na mjeledi.


Hatua za Kuzuia

  • Panda aina za miwa zinazostahimili ugonjwa wa Fugwe.
  • Tumia mimea ya miwa ambayo ina afya ili kuanzisha mimea mipya.
  • Panda mazao tofauti katika eneo moja baada ya muda.
  • Tumia matibabu ya joto kwenye mbegu ili kuua ugonjwa kabla ya kuzipanda.
  • Hii inaweza kufanywa kwa kuweka mbegu kwenye hewa yenye unyevunyevu wa joto la 54°C kwa dakika 150 au maji moto yenye 50°C kwa masaa 2.

Pakua Plantix