Ngano

Kutu ya Mstari wa Njano

Puccinia striiformis

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Upele mdogo, wenye kutu uliopangwa kwa mistari.
  • Shina na vishada/masuke pia vinaweza kuathiriwa.

Inaweza pia kupatikana kwenye

2 Mazao
Shayiri
Ngano

Ngano

Dalili

Ukali wa ugonjwa hutegemea uwezekano wa kuambukizwa wa mmea. Katika aina zenye hatari kubwa ya kuambukizwa, kuvu hutoa upele/ukurutu mdogo, njano hadi machungwa ("kutu") ambayo hupangwa kwa safu na kutengeneza mistari myembamba sambamba na mishipa ya majani. Hatimaye huungana na unaweza kufunika jani zima, dalili inayoonekana mapema katika mimea michanga. Upele huu (0.5 hadi 1 mm kwa kipenyo) wakati mwingine unaweza pia kupatikana kwenye shina na vishada/masuke. Katika hatua za baadaye za ugonjwa, madoa au mistari mirefu ya kahawia nyepesi, yenye tishu zilizo kufa, huonekana kwenye majani, mara nyingi hufunikwa na upele wenye kutu. Katika maambukizi makali, ukuaji wa mimea unaathiriwa sana na tishu zinaharibiwa. Umbo dogo la majani husababisha uzalishaji kupungua, masuke machache kwa kila mmea na punje chache kwa kila suke. Kwa ujumla, ugonjwa huo unaweza kusababisha hasara kubwa ya mazao

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Dawa nyingi za kuua kuvu zinapatikana sokoni. Bidhaa zinazotokana na Bacillus pumilus zinazotumiwa kwa muda wa siku 7 hadi 14 zinafaa dhidi ya kuvu na zinauzwa na watendaji wakuu wa sekta hiyo.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Kunyunyizia majani kwa dawa za kuvu za kundi la strobilurin hutoa ulinzi mzuri dhidi ya ugonjwa endapo zitawekwa kama kinga. Katika mashamba ambayo tayari yameambukizwa, tumia bidhaa za familia ya triazole au mchanganyiko wa bidhaa zote mbili.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa na kuvu Puccinia striiformis, vimelea washirika wanaohitaji nyenzo hai za mimea ili kuishi. Vijimbegu hutawanywa hadi mamia ya kilomita kwa mikondo ya upepo na vinaweza kuanzisha milipuko ya ugonjwa ya msimu. Kuvu huingia kwenye mmea kupitia stomata na hatua kwa hatua hutawala tishu za majani. Ugonjwa huu hutokea hasa mwanzoni mwa msimu wa ukuaji. Hali zinazofaa kwa ukuaji wa kuvu na maambukizi ni mwinuko wa juu, unyevu wa juu (umande), mvua na joto la chini kati ya 7 na 15°C. Maambukizi hukoma wakati halijoto inapozidi 21-23°C kwa sababu kwa halijoto hizi mzunguko wa maisha wa kuvu hukatizwa. Mimea mbadala inayoshambuliwa na kuvu huyu ni ngano, shayiri na ngano nyekundu (rai).


Hatua za Kuzuia

  • Panda aina zinazostahimili magonjwa kama zinapatikana.
  • Hakikisha kuna mbolea ya naitrojeni ya kutosha, epuka matumizi ya naitrojeni kupita kiasi.
  • Chunguza mashamba mara kwa mara kuona mimea ya kujiotea yenyewe na uiondoe.
  • Lima na fukia mabaki ya mazao chini kabisa kwenye udongo baada ya kuvuna.

Pakua Plantix