Ustilago segetum var. tritici
Kuvu
Dalili huonekana muda mfupi kabla au wakati wa kipindi cha maua na una sifa ya masuke meusi na punje nyeusi zenye unga na harufu ya pekee ya "samaki waliooza". Nafasi ya punje zinazokua huchukuliwa na kuvu na hakuna nafaka zinazokua kwenye vichwa vilivyoambukizwa. Ni ugonjwa wa kawaida katika kanda zote za ulimwengu zinazo zalisha ngano. Hasara ya mavuno kwenye vichwa vilivyoambukizwa ni ya moja kwa moja.
Loweka mbegu katika maji ya 20-30 ° C kwa masaa 4-6. Baada ya hapo, tumbukiza kwenye maji moto ya 49°C kwa dakika 2. Katika hatua inayofuata, weka mbegu kwenye karatasi za plastiki na uziweke kwenye mwanga wa jua kwa masaa mengine 4. Mbegu zinapaswa kukaushwa kwa hewa kabisa kabla ya kupanda. Tiba hii inapunguza hatari ya maambukizi. lakini inaweza kuathiri kiwango cha kuota kwa mbegu.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Mbegu zinaweza kutibiwa kwa dawa za kuua kuvu kama vile carboxin au triadimenol, ambazo huchukuliwa na mbegu inayoota na kudhibiti au kuua fangasi ndani ya mbegu. Aina tofauti za dawa zinapatikana ili kutibu mbegu, kati ya nyingi, triticonazole, difenoconazole na tebuconazole.
Dalili husababishwa na fangasi wanaoenezwa na mbegu Ustilago tritici, ambao huishi katika hali bwete ndani ya mbegu za ngano zilizo ambukizwa. Ukuaji wa kuvu huendana na mzunguko wa maisha ya mmea. Mbegu iliyoshambuliwa inapoota, kuvu huanza tena kukua pamoja na vichipukizi vya mimea michanga ya ngano na hatimaye kutawala tishu za maua. Badala ya kutoa chavua, maua hayo hutawanya vijidudu vya kuvu vinavyo enezwa na upepo hadi kwenye maua yenye afya. Huko, kuvu huota na kuanza kutawala tishu za ndani, hatimaye kuingizwa kwenye mbegu mpya. Mbegu zilizoshambuliwa hubeba fangasi bwete lakini huonekana kuwa zina afya. Mzunguko utaanza tena baada ya upandaji wa mbegu hizo. Njia zingine za kutawanya ni pamoja na mabaki ya mavuno, mvua na wadudu. Hali nzuri kwa ajili ya kuota kwa haraka kwa vijimbegu vya kuvu ni hali ya hewa yenye unyevunyevu (60-85% ya unyevunyevu kiasi) na mvua za mara kwa mara au umande na joto la wastani kati ya 16-22°C.