Ngano

Kutu ya Majani ya Ngano

Puccinia triticina

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Malengelenge/upele mdogo wa rangi ya machungwa hadi kahawia kwenye majani.
  • Upele uliozungukwa na ukingo wa manjano.
  • Ala za majani pia zinaweza kuathirika.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Ngano

Dalili

Kutu ya majani ni ugonjwa wa kutu uliozoeleka sana kwenye ngano. Dalili hutegemea uwezekano wa mmea kuathiriwa. Una sifa ya upele mwingi mdogo wa rangi ya machungwa-nyekundu hadi kahawia uliotawanyika kwenye nyuso zote mbili za majani, ala za majani na maganda ya punje za ngano. Una kipenyo cha hadi 1.5 mm, umeinuka kidogo na umbo la mviringo hadi mstatili. Kwenye mimea inayo athiriwa kirahis, chunusi ndogo za upili na halo ya kijani hafifu au ya manjano inaweza kuonekana karibu na upele wa awali. Baada ya muda, rangi hugeuka kuwa kahawia nyeusi au nyeusi. Katika aina za ngano zinazostahimili zaidi, upele wa rangi ya machungwa kawaida huwa mdogo na unaweza kuzungukwa na maeneo ya yaliyo badilika rangi au yenye tishu zilizokufa. Maambukizi husababisha uharibifu wa tishu za mimea, kupoteza maji, na kupungua kwa uzalishaji. Dalili hizi, pamoja na kupunguzwa kwa seti ya maua na kusinyaa kwa punje, huhatarisha mavuno.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Samahani, hatujui matibabu yoyote mbadala dhidi ya Puccinia triticina . Tafadhali wasiliana nasi ikiwa unajua kitu ambacho kinaweza kusaidia kupambana na ugonjwa huu. tunatarajia kusikia kutoka kwako.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Dawa za kunyunyuzia za majani zenye viua kuvu zenye propiconazole au triazole zinaweza kutumika kwa kuzuia ili kuepuka ugonjwa huo. Soma kwa uangalifu maagizo ya jinsi ya kutumia bidhaa. Heshimu nyakati za uwekaji wa dawa na kipimo ili kuzuia ukuaji wa ukinzani.

Ni nini kilisababisha?

Ugonjwa huo husababishwa na kuvu Puccinia triticina, vimelea tegemezi vya tishu za mimea. Vinahitaji mimea hai ya ngano au mwenyeji mbadala ili kukamilisha mzunguko wake wa maisha. Vijimbegu hutawanywa na mikondo ya hewa hadi mamia ya kilomita kutoka kwenye chanzo chao. Mchakato wa kuota unahitaji unyevu wa juu au muda mrefu wa unyevu wa majani na halijoto kati ya 10° na 30°C (16–22°C ni bora zaidi). Katika hali hizi, kuota kwa vijimbegu kunaweza kutokea ndani ya dakika 30 kutoka kwenye mgusaano wa kwanza na jani. Viwango vya juu vya mbolea ya naitrojeni pia ni nzuri. Kuvu huingia kwenye mmea kupitia fursa za asili kwenye majani au ala za jani. Kuvu wanaweza kukamilisha mzunguko wa maisha yao katika siku 7 hadi 8, kulingana na hali ya shamba. Puccinia triticina ana aina mbalimbali za mimea mwenyeji mbadala katika familia ya nafaka.


Hatua za Kuzuia

  • Panda aina thabiti na sugu ikiwa zinapatikana.
  • Panda ngano ya msimu wa baridi kwa kuchelewa na ngano ya majira ya joto mapema kuliko kawaida.
  • Kagua sehemu za mashamba kama kuna mimea iliyo ota yenyewe na uiondoe.
  • Hakikisha kuna msongamano mdogo wa mazao wakati wa kupanda.
  • Panga na tekeleza mzunguko mzuri wa mazao.
  • Hakikisha mbolea ya kutosha ya naitrojeni.
  • Ondoa na uharibu mabaki ya mazao baada ya kuvuna.

Pakua Plantix