Mpunga

Ukungu Mkuu wa Mpunga

Magnaporthe oryzae

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa meupe yenye umbo la duara au mviringo na kingo nyeusi kwenye majani.
  • Vifundo vya shina pia vinaweza kuonyesha dalili.
  • Kufa kwa miche au mimea michanga.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Mpunga

Dalili

Ukungu mkuu wa mpunga huathiri sehemu zote za juu ya ardhi za mmea: jani, shina, Vifundo, pingili, sehemu za masuke, na wakati mwingine vikonyo vya majani. Majani huonyesha rangi ya manjano au kijani mpauko, vidonda vya umbo la jicho na ncha zilizochongoka. Mipaka ya vidonda hivi huwa na seli zilizokufa na katikati huwa na rangi ya kijivu hadi nyeupe. Ukubwa wa vidonda hutegemea umri wa mmea, aina ya mbegu na wakati wa maambukizi. Wakati vidonda vinakua, majani huuendelea kukauka hatua kwa hatua . Ikiwa makutano ya majani na vikonyo yameambukizwa, kuoza kwa kola kunaweza kuonekana, na majani yaliyo juu ya makutano hufa. Vifundo vya shina pia vinaweza kuathiriwa. Hii husababisha vifundo vya shina kuwa vya kahawia na kuvunjika kwa shina, mara kwa mara na kusababisha kifo kamili cha miche au mimea michanga. Katika hatua za ukuaji wa baadaye, maambukizi makali ya ukungu mkuu hupunguza eneo la majani na hivyo kuathiri mavuno.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hadi leo, hakuna njia madhubuti za kibayolojia za kudhibiti ugonjwa huu ambazo zinapatikana kibiashara. Majaribio yanaendelea ili kupima uwezo wa bidhaa zenye bakteria aina ya Streptomyces au Pseudomonas kwenye kupambana na kuvu au kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Tibu mbegu zako na thiram, hufaa dhidi ya ugonjwa huu. Dawa za kuua kuvu zilizo na azoxystrobin, au viambato amilifu vya familia ya triazoli au strobilurins pia vinaweza kupuliziwa katika hatua ya vitalu, kulima, kupanda na kuchanua ili kudhibiti ugonjwa wa ukungu mkuu wa mpunga. Matumizi mara moja au mbili ya dawa ya kuua kuvu kwa msimu yanaweza kuwa na ufanisi katika kudhibiti ugonjwa huu.

Ni nini kilisababisha?

Dalili za ukungu mkuu wa mpunga husababishwa na fangasi anaejulikana kama Magnaporthe grisea, ambao ni moja ya magonjwa hatari zaidi ya mpunga. Ugonjwa huu unaweza pia kuathiri nafaka nyingine muhimu za kilimo kama vile ngano, shayiri, na mtama wa lulu. Kuvu/fangasi hawa wanaweza kuishi kwenye mabua au majani makavu baada ya kuvuna na hivyo kubebwa hadi msimu ujao. Mimea kwa kawaida huwa haishambuliwi sana na ugonjwa huu inapokomaa. Ugonjwa huu hupendelea joto la wastani, mvua za mara kwa mara, na unyevu mdogo wa udongo. Kipindi cha muda mrefu cha unyevu wa majani pia husababisha maambukizi. Katika mpunga wa nyanda za juu, maeneo ambayo huwa na umande (tofauti kubwa ya joto la mchana na usiku) yako hatarini pia. Hatimaye, mimea iliyopandwa kwenye udongo wenye naitrojeni nyingi au viwango vya chini vya madini ya silikoni ina uwezekano mkubwa wa kuathiriwa na ugonjwa huu.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia mbegu bora zenye afya au zilizo thibitishwa.
  • Panda aina ya mbegu stahimilifu (zinastahimili magonjwa) zinazopatikana katika eneo lako.
  • Panda mbegu mapema wakati wa msimu, baada ya msimu wa mvua kuanza.
  • Epuka matumizi ya mbolea zenye kiasi kikubwa cha naitrojeni na ugawanye mbolea kwa kuweka mara mbili au zaidi.
  • Hakikisha mimea yako haipati ukame kwa kumwagilia mara kwa mara.
  • Ruhusu kiwango sahihi cha maji ili mpunga ukue vizuri.
  • Endelea kuruhusu maji mara kwa mara kwenye shamba na funga mifereji itakayo toa maji kwenye shamba la mpunga.
  • Dumisha udhibiti wa magugu na mimea mingine inayoweza kuhifadhi magonjwa ya mpunga.
  • Weka mbolea zenye silikoni ikiwa udongo unajulikana kuwa na upungufu wa madini hayo.
  • Vyanzo mbadala vya madini ya silikoni ni pamoja na mabua ya mpunga yenye silikoni nyingi.
  • Fuatilia eneo lako mara kwa mara ili kugundua dalili za magonjwa.
  • Angamiza mabaki yote ya mimea iliyoambukizwa ili kuzuia mwendelezo wa magonjwa shambani.
  • Panga mzunguko wa mazao kama njia rahisi na nzuri ya kupunguza idadi ya vimelea vya magonjwa.

Pakua Plantix