Puccinia arachidis
Kuvu
Kutu ya karanga huonekana kama upele mdogo wa mviringo wenye rangi ya kahawia ya chungwa (kutu), mara nyingi kwenye upande wa chini wa majani. Upele huo mara nyingi huzungukwa na mduara wa njano. Hii hupunguza ukuaji wa majani na mmea kwa kiasi kikubwa. Ugonjwa unapoendelea, majani yaliyoathiriwa sana hufunikwa na upele/ukurutu wa kutu pande zote mbili, kugeuka njano na "yenye kutu", na hatimaye kusinyaa. Upele ulio refuka, wenye rangi ya kahawia nyekundu (na baadae mweusi) unaweza kuonekana kwenye mashina na vikonyo. Upukutishaji wa majani unaweza kutokea baadaye. Ugonjwa huu unaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa mavuno ya karanga na malisho na ubora wa mafuta.
Mawakala wa kibaolojia wanaweza kusaidia kudhibiti maambukizi. Viziduo vya mimea ya Salvia officinalis na Potentilla erecta vina uwezo wa kinga kwenye majani dhidi ya ukuaji wa kuvu. Viziduo vingine vya mimea kama vile mafuta ya mbegu za kitani na mafuta ya karanga pia vimekuwa na ufanisi katika kupunguza matukio ya ugonjwa huu.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Matibabu ya kemikali yanaweza kushindikana katika hatua za baadaye za maendeleo ya ugonjwa huo. Iwapo dawa za kuua kuvu zinahitajika, nyunyiza bidhaa zenye mancozeb, propiconazole au chlorothalonil (3gramu/lita ya maji). Matumizi yanapaswa kuanza moja kwa moja baada ya kuonekana kwa mara ya kwanza kwa maambukizi na yanapaswa kurudiwa baada ya siku 15.
Kutu ya karanga huishi kwenye mabaki ya mazao kwenye udongo au kwenye mimea mingine jamii ya mikunde ambayo hutumika kama mwenyeji mbadala. Maambukizi ya awali ni kutokana na vijimbegu vinavyo zalishwa katika hatua hii ya uzaaji na kutua kwenye upande wa chini wa majani. Ueneaji wa upili hutokea wakati vijimbegu vinaposambazwa na upepo. Sehemu zilizo ambukizwa zinaweza kupanuka haraka wakati wa hali ya mazingira ni rafiki kwa ukuaji wa kuvu, kwa mfano, hali joto (21 hadi 26 ° C) na hali ya hewa ya mvua, ya mawingu (ukungu au umande mkubwa wa usiku). Pia hukandamiza ukuaji wa shina na mizizi ya mmea, na kusababisha ukuaji ulio dumaa. Kiasi kikubwa cha mbolea ya fosforasi kwenye udongo kinaonekana kupunguza kasi ya ukuaji wa kutu.