Mycosphaerella
Kuvu
Madoa ya mviringo kwenye pande zote za majani. Doajani wahi huwa na sifa ya vidonda laini vya rangi ya kahawia nyepesi, ambavyo mara nyingi huzungukwa na mduara angavu wa manjano. Doajani chelewa huwa na sifa ya vidonda vya kahawia iliyokolea au vyeusi na mduara angavu huwepo mara chache. Ugonjwa unapoendelea, madoa hugeuka kuwa meusi na kukua zaidi (hadi 10 mm), na huanza kuonekana kwenye majani ya juu, mashina na vigingi. Kwa upande wa Doajani wahi, ukuaji wa kuvu wa rangi ya fedha, wenye umbo kama nywele wakati mwingine unaweza kuonekana sehemu ya juu ya jani. Ikiwa hali ya mazingira ni rafiki, majani hatimaye hudondoka na mashina na vigingi hudhoofika. Upukutishaji majani hudhoofisha mmea na uzalishaji wake. Hasara za mavuno huongezeka kadiri vigingi vilivyoambukizwa kupoteza nguvu na kuvunjika wakati wa kuvuta na kupura wakati wa kuvuna.
Bakteria wa kuzuia fangasi Bacillus circulans na Serratia marcescens wanaweza kutumika kwenye majani ili kupunguza matukio ya doajani chelewa kwenye majani ya karanga.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia. Dawa za kuua kuvu zenye chlorothalonil, tebuconazole, propiconazole azoxystrobin, pyraclostrobin, fluoxastrobin au boscalid zinaweza kutumika kama dawa za majani kudhibiti magonjwa yote mawili. Kwa mfano, kunyunyizia 3gramu/lita mancozeb au 3gramu/lita chlorothalonil dalili zinapoanza kuonekana na ikibidi kurudia dawa baada ya siku 15.
Madoajani chelewa na wahi ni magonjwa mawili tofauti yenye dalili zinazofanana ambazo huonekana katika hatua tofauti za ukuaji wa mmea, na hivyo majina yake husika. Husababishwa na fangasi Mycosphaerella arachidis (doajani wahi) na Mycosphaerella berkeleyi (doajani chelewa). Mimea ya karanga ndiyo mimea pekee inayojulikana kushambuliwa na magonjwa haya. Chanzo kikuu cha uambukizaji ni mabaki ya mazao ya awali ya karanga. Unyevu mwingi (umande), mvua nyingi (au umwagiliaji wa juu) na halijoto (zaidi ya 20 ° C) kwa muda mrefu huhamasisha maambukizi na kuendelea kwa ugonjwa huo. Madoajani chelewa na wahi ni magonjwa hatari zaidi ya karanga duniani kote na yanaweza kusababisha hasara kubwa ya mavuno ya karanga, mojawapo au yote kwa pamoja.