Mahindi

Muozo Mwekundu

Glomerella tucumanensis

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa mekundu kwenye mabua/mashina, majani.
  • Nafaka zilizobadilika rangi, zilizooza.
  • Kunyauka na kukunjamana kwa majani.
  • Harufu mbaya.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Mahindi

Dalili

Mabua/mashina yaliyoambukizwa yana rangi ya kufifia na huonyesha madoa makubwa mekundu juu ya uso. Sehemu ya urefu wa bua/shina inaonyesha tishu nyekundu zilizooza kwenye kiini cheupe. Katika mimea sugu, maeneo mekundu, yenye ugonjwa mara nyingi hutokea kwenye vifundo. Ugonjwa unapoendelea, vijishimo vinaweza kuundwa ndani ya kiini na vitita vya nyuzi ngumu huonekana pia. Majani hunyauka na kusinyaa. Mimea huanza kutoa harufu mbaya na mabua/mashina huvunjika kwa urahisi chini ya hali mbaya ya hewa. Kwenye majani, vidonda vidogo vya mviringo vyekundu au vilivyo refuka vinakua kwenye mshipa mkuu wa katikati, wakati mwingine kwa urefu wake kamili. Vifukojani vinaweza kuwa na mabaka mekundu na madoa madogo meusi hukua mara chache kwenye ubapa wa majani.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Ulowekaji kwenye maji ya moto (kwa mfano 50°C kwa saa 2) unaweza kutumika kuua vimelea kwenye mbegu na kudhibiti matukio ya muozo mwekundu. Mawakala wa udhibiti wa kibayolojia pia wanaweza kutumika kutibu mbegu. Hawa ni pamoja na aina za fangasi wa jenasi Chaetomium na Trichoderma na baadhi ya spishi za bakteria Pseudomonas. Dawa za kunyunyuzia majani zenye vimiminika hivi pia zinafaa katika kupunguza kuenea kwa ugonjwa huo.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi yenye hatua za kinga na matibabu ya kibayolojia ikiwa inapatikana. Tibu mbegu kwa maji ya moto yaliyochanganywa na dawa ya kuvu katika 50-54°C kwa saa 2 ili kuua vimelea (kwa mfano, thiram). Matibabu ya kemikali shambani hayana ufanisi na hayashauriwi.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa na fangasi waitwao Glomerella tucumanensis, ambao wanaweza kuishi kwa muda mfupi tu (miezi) kwenye udongo. Ingawa sio vimelea halisi vinavyo enezwa na udongo, vijimbegu vilivyooshwa kwenye udongo kutoka kwa uchafu wa mazao vinaweza kuzalisha maambukizi katika mbegu au miche iliyopandwa hivi karibuni. Baada ya hapo, ugonjwa huenea kupitia vijimbegu vinavyo zalishwa katikati ya mimea au mabua ya mimea iliyoambukizwa na kusafirishwa kwa upepo, mvua, umande mzito, na maji ya umwagiliaji. Baridi, hali ya hewa ya mvua, unyevu wa juu wa udongo na kilimo cha zao moja hupendelea ugonjwa huo. Ukame pia huongeza uwezekano wa mmea kushambuliwa. Mbali na miwa, fangasi pia huweza kuambukiza mazao kama mahindi na mtama kwa kiasi kidogo.


Hatua za Kuzuia

  • Panda aina sugu, ikiwa zinafaa kwa eneo lako.
  • Tumia mbegu na miche yenye afya kutoka kwenye chanzo kilichoidhinishwa.
  • Pata nyenzo za upanzi kutoka kwenye mashamba yasiyo na magonjwa.
  • Badilisha wakati wa kupanda ili kuepuka hali ya joto sana au baridi sana wakati wa msimu.
  • Fuatilia shamba mara kwa mara na ondoa mimea iliyo na magonjwa.
  • Epuka machipukizi ya mazao yenye magonjwa.
  • Ondoa uchafu wowote wa mimea shambani baada ya kuvuna na uchome moto.
  • Vinginevyo, kulima shamba mara kadhaa ili kufichua kuvu waliomo kwenye udongo kwa mwanga wa jua.
  • Panga mzunguko mzuri wa mazao na mimea isiyoweza kuambukizwa kwa miaka 2-3.

Pakua Plantix