Sphacelotheca reiliana
Kuvu
Dalili za kwanza za ugonjwa huonekana katika hatua za baadaye za ukuaji wa mmea, wakati kuchanua. Ukuaji wa kuvu/fangasi weusi, ulio mithili ya unga unafunika sehemu ya shada la maua(mbelewele) au shada zima. Maumbile yasiyo ya kawaida yanayofanana na majani yanaweza kuonekana kwenye mashada ya maua au masikio ya mahindi. Masikio yaliyoathirika yanakuwa ni ya mviringo zaidi ukilinganisha na yale yenye afya na yanakuwa yamejaa kabisa na mkusanyiko ya ungaunga mweusi. Msongamano wa nyuzi za mishipa ya majani ambao ni mabaki ya tishu ngumu za mmea huchanganyika katikati ya makundi ya vijimbegu (viiniyoga) vya kuvu. Kwa kawaida mimea iliyoathirika haina ndevu za mahindi au punje kwenye masikio. Kuota matawi kupita kiasi kunaelezwa kama dalili ya pili.
Mbawakavu wanaokula kuvu (m.f Phalacrus obscurus na Lystronychus coeruleus) wanaweza kutumika kama wadudu wa kudhibiti kuvu kibaiolojia. Matibabu ya mbegu kwa kutumia viziduo (extracts) vya bakteria aina Bacillus megaterium pia inaweza kupunguza uwezekano wa ugonjwa kujitokeza.
Daima zingatia mbinu jumuishi zinazotumia hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaiolojia ikiwa zinapatikana. Mbegu zinaweza kutibiwa na dawa ya kuua kuvu inayofyonzwa na mbegu (carboxin) ili kuzuia kuvu kuambukiza mimea, ingawaje njia hii udhibiti wake ni wa kiwango kidogo tu. Matibabu ya dawa za kuua kuvu kwenye mashimo wakati wa hatua ya miche yanaweza pia kuwa na ufanisi, lakini yanaweza yasiwe na faida kiuchumi.
Kuvu aina ya Sphacelotheca reiliana wanaweza kuishi kama vijimbegu (viiniyoga) kwenye udongo kwa miaka kadhaa na huambukiza kipekee kupitia mizizi. Mara chache huambukiza baadhi ya mimea shambani, hususani katika hatua ambayo mimea bado ni miche. Baadaye, kuvu hukua kwenye sehemu zote za mmea, ikiwemo maua (shada) na masikio. Hii huonekana kama ukuaji wa fugwe mweusi (makundi ya vijimbegu/viiniyoga vya kuvu) ambavyo hula mashada na wakati mwingine huchukua nafasi ya punje kabisa. Maambukizi kutoka shamba moja hadi lingine yanaweza kutokea kupitia vifaa vya kilimo vyenye vimelea. Unyevu wa chini wa udongo, joto la wastani (21 hadi 27°C), na upungufu wa virutubisho huongeza uwezekano wa maambukizi na ukuaji wa ugonjwa. Mara maambukizi yanapotokea, kunakuwa hakuna matibabu yenye ufanisi ya kupunguza uharibifu kwenye mimea iliyoathirika.