Kitunguu maji

Kutu ya Kitunguu Mwitu

Puccinia porri

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa madogo meupe huonekana pande zote mbili za majani.
  • Madoa hukua na kuwa malengelenge angavu ya kutu ya rangi ya chungwa.
  • Uso wa majani huonyesha matundu yanayofanana na mipasuko.
  • Maambukizi makali husababisha mmea kwa wa njano, kunyauka na kukauka.
  • Balbu za vitunguu saumu zinaweza kunyauka na kuwa na ubora wa chini.

Inaweza pia kupatikana kwenye

2 Mazao
Kitunguu saumu
Kitunguu maji

Kitunguu maji

Dalili

Maambukizi yanaweza kutokea katika hatua yoyote ya ukuaji na huonekana kwanza kwenye majani. Dalili za awali huonekana kama madoa madogo meupe ambayo yanaweza kuwepo pande zote za bapa ya jani(lamina). Baada ya muda, madoa haya hukua na kuwa malengelenge angavu ya kutu ya rangi ya chungwa ambayo yanahusiana na miundo inayozalisha vijimbegu. Kadiri upele/ukurutu unavyoendelea kukua, hupasuka ili kutoa vijimbegu. Majani hatimaye hugeuka rangi kwa manjano na vidonda vinaweza kujitokeza kwenye urefu wa bapa ya jani (lamina), wakati mwingine kusababisha matundu yanayofanana na mpasuko. Katika hali ya maambukizi makali, mimea yote hugeuka manjano na kunyauka, hali ambayo inaweza kusababisha mimea kufa mapema. Kama mimea itaathiriwa mapema, au ikiwa maambukizi makali yanatokea, vitunguu vidogo na vilivyo sinyaa vyenye ubora wa chini vitazalishwa.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Kuzuia ndio njia pekee ya kukabiliana na kutu kwa muda mrefu. Baadhi ya michanganyiko iliyo na salfa huchukuliwa kuwa hai na inaweza kutumika kwa njia ya kuzuia ili kupunguza hatari ya kuambukizwa. Kuna njia tofauti za uwekaji, kwa mfano poda ya salfa inaweza kunyunyiziwa au kumwaga kama vumbi kwenye mimea. Au salfa iliyochanganywa na maji inaweza kutumika kama dawa ya kunyunyizia majani au kumwaga kwenye udongo karibu na kitako cha mmea. Kwa matumizi sahihi, tafadhali fuata mwongozo wa bidhaa husika au muulize mfanyabiashara wa eneo lako.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia, ikiwa yanapatikana. Bidhaa zilizo na azoxystrobin au mancozeb zinaweza kutumika kama dawa ya kuzuia majani au upakaji udongo ili kuzuia hatari ya kuambukizwa. Tafadhali kumbuka kuwa haiwezekani kutibu ugonjwa huu wa kuvu.

Ni nini kilisababisha?

Ugonjwa huo husababishwa na kuvu Puccinia porri, ambae anaweza kuishi tu kwenye tishu hai za mimea. Ni lazima akae kwenye mimea mbadala (magugu au mimea ya kujiotea yenyewe) kwa kipindi chote cha majira ya baridi kali, au azae vijimbegu ili kupitisha msimu bwete (dormant season). Vijimbegu hivi vya fangasi husafirishwa kwa upepo na matone ya mvua hadi kwenye mimea au mashamba mengine. Unyevu mwingi, mvua ya chini na joto kati ya 10-20 ° C ni hali rafiki zaidi kwa mzunguko wa maisha ya kuvu na kuenea kwa ugonjwa huo. Katika hali hizi, mara tu vijimbegu vya kuvu vikitua kwenye mimea mwenyeji, kuvu hukua na kuanza kuutawala mmea. Muda kati ya maambukizi na mlipuko wa ugonjwa ni kati ya siku 10-15, kulingana na joto na viwango vya unyevu. Wakati mwafaka wa kuenea ni mwishoni mwa majira ya joto. Ugonjwa huo unaweza kusababisha hasara kubwa ya mavuno na unaweza kupunguza uwezekano wa kuhifadhi vitunguu.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia mbegu zenye afya au malighafi za upanzi kutoka kwenye chanzo kilichoidhinishwa.
  • Fuata nafasi zinazopendekezwa za kupanda kwa mistari ili kuhakikisha mzunguko wa hewa mzuri na kuepuka kuenea kwa ugonjwa huo.
  • Chagua maeneo ya upandaji yasiyo tuamisha maji, hakikisha mashamba yana mifumo mizuri ya kupitisha maji na usimwagilie maji kupita kiasi.
  • Hakikisha unashughulikia kwa uangalifu wakati wa kupalilia ili kuepuka kuharibu kitunguu.
  • Usipande mimea ya familia ya allium katika udongo wenye naitrojeni nyingi.
  • Tumia mbolea zenye potasiamu ya kutosha (kwa mfano salfeti ya potashi).
  • Inashauriwa kumwagilia asubuhi ili kuepuka hali ya unyevu wakati wa usiku.
  • Angalia mimea au mashamba yako mara kwa mara ili kuona dalili zozote za ugonjwa.
  • Ondoa mimea iliyoambukizwa mara baada ya dalili za awali kuonekana na uiharibu kwa kuchoma au vinginevyo.
  • Panga mzunguko wa mazao na mazao yasiyo hifadhi/kushambuliwa na ugonjwa huu kwa angalau miaka 2-3.
  • Haribu mimea jamii ya vitunguu (allium) ambayo huota yenyewe wakati huo ili kuhakikisha maeneo ya upandaji yasiyo na vimelea.
  • Takasa vifaa na zana zako na osha mikono yako mara kwa mara ili usisambaze ugonjwa huo kati ya mashamba.

Pakua Plantix