Phytophthora infestans
Kuvu
Madoa ya kijani-Kahawia huonekana kwenye kingo za majani na upande wa juu wa majani. Baada ya hapo sehemu kubwa ya majani hugeuka kuwa ya kahawia kabisa. Wakati wa hali ya hewa ya unyevu vidonda kwenye upande wa chini wa majani vinaweza kufunikwa na ukungu wa kijivu au mweupe, na kufanya iwe rahisi kutofautisha majani yenye afya na yale yenye tishu zilizokufa. Ugonjwa unapoendelea, majani huwa ya kahawia, hujikunja na kukauka. Wakati mwingine madoa ya kahawia yaliyosambaa zaidi na kufunikwa na ukungu mweupe pia huonekana kwenye mashina, matawi na vikonyo vya majani. Madoa ya kijivu-kijani hadi kahawia iliyochafuka na mikunjo huonekana kwenye matunda. Kwenye maeneo ya madoa haya, nyama ya tunda huwa ngumu.
Mpaka sasa, hakuna udhibiti wa kibayolojia wenye ufanisi unaojulikana dhidi ya ugonjwa wa Bakajani Chelewa/Ukungu Chewa. Ili kuzuia kuenea, ondoa na uharibu mimea iliyo ambukizwa mara moja na usiitumie mimea iliyoambukizwa kutengeneza mboji.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na udhibiti wa kibayolojia ikiwa unapatikana. Tumia dawa za kunyunyiza za kuua vimelea zenye mojawapo ya kemikali hizi mandipropamid, chlorothalonil, fluazinam, mancozeb ili kukabiliana na ugonjwa wa Bakajani Chelewa/Ukungu Chelewa. Dawa za kuua kuvu zitahitajika endapo ugonjwa utaonekana msimu ambao kuna uwezekano wa mvua au umwagiliaji wa juu unafanywa.
Hatari ya kuambukizwa kwa ugonjwa huu ni kubwa zaidi katikati ya msimu wa joto. Kuvu huingia kwenye mmea kupitia majeraha na nyufa kwenye ngozi. Joto na unyevu ni hali za kimazingira zinazo chochea zaidi maendeleo ya ugonjwa huo. Kuvu anaesababisha ugonjwa wa Bakajani Chelewa/Ukungu Chelewa hukua vyema katika unyevu wa juu (karibu 90%) na katika viwango vya joto vya 18 hadi 26°C. Hali ya hewa ya joto zaidi na kavu inaweza kukomesha kuenea kwa ugonjwa huu.