Kiazi

Koga ya Rangi ya Fedha

Helminthosporium solani

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa madogo ya kijivu cha fedha au vidonda vinavyoongezeka kuwa miduara.
  • Kawaida hayana umbo maalumu na hutokea nchani/mwishoni mwa kiazi.
  • Vidonda kawaida hubaki juu juu bila kusababisha uharibifu kwa tishu za ndani zaidi.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Kiazi

Dalili

Dalili kawaida huonekana wakati wa kuvuna, lakini ugonjwa hujitokeza wakati wa kuhifadhi. Wakati wa kuhifadhi, viazi huonyesha madoa ya rangi ya fedha ambayo hukua hadi kwenye miduara yenye ukingo dhahiri wa kahawia. Vidonda baadaye huunganika na vinaweza kugeuka kuwa kahawia, na kufanya iwe vigumu kuonekana kwenye viazi ambavyo havijaoshwa. Kuonekana kwa vidonda pia hutofautiana na aina ya viazi, hasa kutokana na aina za ngozi. Tabaka la nje la ngozi ya viazi vilivyoambukizwa hulainika na kukunjamana na hatimaye kuchubuka. Maambukizi ya upili na vimelea vingine yanaweza kutokea.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Dawa za asili za kuua viumbe hai (hydrogen peroxide) au bidhaa za kibayolojia za (Bacillus subtilis, mafuta ya karafuu) zimeonyesha ufanisi mdogo au kukosekana kabisa katika kupunguza hatari ya maambukizi ya koga ya rangi ya fedha.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Uwekaji wa dawa za kuua kuvu kwenye mbegu za viazi kabla ya kupandwa au wakati wa kuvuna kunaweza kuzuia maambukizi. Thiabendazole, inayotumiwa kwenye viazi kama vumbi, inaweza kupunguza matukio ya koga ya rangi ya fedha katika msimu unaofuata au wakati wa kuhifadhi.

Ni nini kilisababisha?

Koga ya rangi ya fedha husababishwa na fangasi wanaoenezwa na mbegu waitwao Helminthosporium solani. Wanaishi kwenye mizizi kwa muda mrefu na huambukiza ngozi. Maambukizi yanaweza kutokea kutoka kwenye udongo, matumizi ya viazi vya mbegu vilivyoambukizwa au vimbegu vya kuvu vilivyobaki katika vyumba vya kuhifadhi. Joto la 3 ° C na unyevunyevu chini ya 90% wakati wa kuhifadhi huzuia maendeleo ya ugonjwa huo. Uwepo wa vitu vilivyo ganda kwenye viazi wakati wa kuhifadhi (hewa ya joto hukutana na viazi baridi) huongeza tatizo. Ingawa viazi bado vinaweza kuliwa, thamani yake sokoni hupunguzwa sana.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia mbegu kutoka kwa mimea yenye afya au kutoka kwa vyanzo vilivyoidhinishwa.
  • Chagua aina za viazi zinazostahimili.
  • Tekeleza mzunguko mpana wa mazao.
  • Kuinulia mizizi mapema hupunguza matukio.
  • Dhibiti mimea inayojiotea yenyewe baada ya kuvuna.
  • Safisha na takasa zana na vifaa vya kazi kati ya vitalu.
  • Hifadhi viazi katika hali ya baridi na kavu kila wakati, na uingizaji hewa mzuri.
  • Usafi mzuri wa mazingira na shughuli za kuchambua baada ya mavuno ni muhimu.

Pakua Plantix