Kiazi

Koga Nyeusi

Rhizoctonia solani

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa meusi magumu yaliyoinuka kwenye uso wa kiazi.
  • Madoa ya kahawia, yaliyozama na ukungu mweupe wa kuvu kwenye mizizi ya juu na machipukizi mapya.
  • Kunyauka na kubadilika rangi kwa majani.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Kiazi

Dalili

Madoa meusi yaliyoinuka, yasiyo ya kawaida kwa ukubwa au umbo, yanaonekana kwenye uso wa tunguu la viazi (scurfs). Alama hizi nyeusi zinaweza kusuguliwa au kung'olewa kwa urahisi. Kwa msaada wa lens ya mkono, nyenzo nyeupe za kuvu zinaweza kuonekana karibu na madoa haya. Kuvu pia husababisha dalili zinazofanana na zile za kikwachu/donda la shina kwenye machipukizi na mashina mapya. Madoa ya kahawia, yaliyozama hukua kwenye mzizi/tunguu, mara nyingi huzungukwa na ukuaji wa ukungu mweupe. Ikiwa uozo hufunga/kuguguna shina na kuzuia usafirishaji wa maji na virutubisho, majani hubadilika rangi na kunyauka.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Weka dawa ya kuua kuvu ya kibayolojia Trichoderma harzianum, au spishi za Rhizoctonia zisizo na vimelea kwenye mitaro. Hii inaweza kupunguza matukio ya koga nyeusi katika mashamba na idadi ya viazi vilivyoambukizwa. Uwezekano mwingine unaweza kuwa kuweka samadi ya ng'ombe kwenye mitaro au ufukizaji wa kibaiolojia na mabaki ya haradali ya kijani kibichi.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Matibabu ya mbegu na fluodioxinil au mchanganyiko wa thiophanate-methyl na mancozeb yanafaa dhidi ya kuenea kwa magonjwa mbalimbali ya vimelea, kati yao koga nyeusi. Matibabu ya ndani ya mitaro wakati wa kupanda na fluotanil au azoxystrobin pia husaidia kudhibiti ukuaji wa kuvu.

Ni nini kilisababisha?

Koga nyeusi husababishwa na fangasi wa Rhizoctonia solani. Kwa joto la kuanzia 5 hadi 25 ° C, kuvu huishi kwenye udongo kwa muda mrefu, hata bila uwepo wa viazi. Maambukizi yanaweza kutokea kwenye udongo au kwa kutumia viazi vilivyoambukizwa kama nyenzo ya mbegu. Kuvu huyu kiuhalisia hasababishi kuoza, lakini viazi havipaswi kutumiwa kama mbegu. Maambukizi yanaweza kuzidishwa na hali ya hewa ya baridi na ya mvua. Hali ya joto katika hatua za mwanzo za ukuaji wa mmea hupunguza athari za ugonjwa huo. Koga nyeusi na kikwachu/donda la shina pia huwa ni vya kawaida zaidi kwenye udongo mwepesi, na mchanga.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia nyenzo za mbegu kutoka kwenye mimea yenye afya au kutoka kwenye vyanzo vilivyoidhinishwa.
  • Epuka kupanda mapema katika msimu wa joto.
  • Panda mizizi ya mbegu kwenye udongo wenye joto (juu ya 8°C).
  • Zingatia matumizi ya mitaro ya kina kifupi kuruhusu chipukizi kuchomoza mapema kutoka kwenye udongo.
  • Fanya mzunguko wa mazao.
  • Acha mabaki ya mimea isiyohifadhi kuvu kwenye udongo baada ya kuvuna.
  • Mwagilia mimea vya kutosha, haswa wakati wa kiangazi.

Pakua Plantix