Phytophthora infestans
Kuvu
Mabaka/madoa ya kahawia iliyokolea hukua kwenye majani kuanzia kwenye ncha au kingo za majani. Katika hali ya hewa ya unyevunyevu, madoa haya huwa vidonda vyenye maji maji. Utando mweupe wa kuvu unaweza kuonekana kwenye sehemu ya chini ya majani. Ugonjwa unapoendelea, majani yote hunyauka, hugeuka kahawia na kufa. Vidonda hivyo pia hutokea kwenye shina na vikonyo vya majani. Viazi huwa na madoa ya rangi ya kijivu-bluu kwenye ngozi na nyama yake pia hubadilika kuwa kahawia, hivyo basi visiweze kuliwa. Kuoza kwa sehemu ya kiazi iliyoshambuliwa hutoa harufu ya tofauti.
Tumia dawa za ukungu zenye shaba kabla ya hali ya hewa kavu. Dawa za kupuliza za majani zenye uwezo wa kuweka utando hai pia zinaweza kuzuia maambukizi.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na udhibiti wa kibayolojia ikiwa unapatikana. Uwekaji wa dawa za ukungu ni muhimu ili kudhibiti Bakajani/Ukungu Chelewa wa viazi mviringo, hasa katika maeneo yenye unyevunyevu. Dawa za ukungu zinazoua kwa kugusa zinazosambaa kwenye majani zinafaa na hazichochei upinzani wa kuvu kwa dawa. Dawa za kuua kuvu zenye kemikali za mandipropamidi, klorothalonil, fluazinam, au mancozeb pia zinaweza kutumika kama matibabu ya kuzuia. Kutibu mbegu kabla ya kupanda na dawa za kuua kuvu kama vile mancozeb pia hufanya kazi.
Kuvu hawa ni vimelea tegemezi kwa mimea waliyopo. Hii ina maana kwamba baada ya kuvuna ni lazima wabaki katika masalia ya mazao na pia kwenye mimea mbadala ili kuishi majira yote ya baridi. Huingia kwenye mmea kupitia majeraha na nyufa kwenye ngozi. Chavua za kuvu huota kwenye joto la juu wakati wa masika na kuenea kwa upepo au maji. Ugonjwa huu huzidi nyakati za usiku wa baridi (chini ya 18°C), siku za joto (18-22°C), na hali ya unyevunyevu iliyozidi kama vile mvua na ukungu (90% ya unyevunyevu). Katika hali hizi, ugonjwa wa Bakajani Chelewa la Viazi Mviringo linaweza kutokea.