Ustilago maydis
Kuvu
Sehemu zote za mmea zinazokua zinaweza kuambukizwa na kuvu huwa. Uwezekano wao wa kuweza kujeruhiwa na kuweza kukua husababisha sehemu hizo za mmea ziweze kuonyesha dalili kali zaidi. Mimea iliyo katika hatua ya miche ndiyo iliyo hatarini zaidi kupata maambukizi. Katika hali hiyo, ukuaji wa mmea hudumaa na huenda isizalishe maua au masuke. Kwa mimea mikubwa, maambukizi husababisha ukuaji wa uvimbe, ambao ni mchanganyiko wa tishu za mmea uliohifadhi vijidudu pamoja na tishu za kuvu/ukungu. Uvimbe wa fugwe unakuwa na rangi ya kijani yenye weupe katika hatua za awali na hugeuka kuwa mweusi inapokomaa. Ni sifa maalum kwenye masuke, ambapo kila punje moja ya mahindi inaweza kuunda uvimbe wake. Uvimbe huo unapopasuka, hutoa vitu mithili ya unga unga mweusi. Kwenye majani, uvimbe kwa kawaida hubaki mdogo na hukauka bila kupasuka.
Udhibiti wa moja kwa moja wa kuvu/ ukungu ni mgumu na hadi sasa hakuna mbinu yenye ufanisi dhidi ya vimelea hivi vya kuvu.
Wakati wote zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia yanayowezekana. Matumizi ya dawa za kuua kuvu kwenye mbegu na majani hayawezi kupunguza kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa fugwe kwenye mahindi.
Ugonjwa wa fugwe kwenye mahindi unasababishwa na kuvu aitwae Ustilago maydis, ambao wanaweza kubaki kwenye udongo kwa miaka kadhaa. Vijimbegu (viiniyoga) vya kuvu huenea kwenye mimea kupitia upepo, vumbi la udongo na matone ya mvua. Mchakato wa maambukizi unafanikishwa na uwepo wa majeraha kwenye mmea, kama yale yanayosababishwa na wadudu, wanyama, mbinu mbaya za kilimo au mvua ya mawe. Hakuna maambukizi ya pili ya moja kwa moja ya kutoka mmea mmoja hadi mwingine. Dalili huwa kubwa zaidi kwenye tishu zenye uwezekano mkubwa wa kukua (kama vile masuke au ncha zinazokua). Hali mbaya ya hewa inayosababisha uzalishaji mdogo wa chavua na viwango duni vya uchavushaji (kama vile ukame unaofuatiwa na mvua kubwa) inachangia kuenea kwa ugonjwa huu.