Fusarium oxysporum
Kuvu
Kuvu/fangasi huyu huonesha mpangilio maalum wa uharibifu wa mazao. Katika baadhi ya matukio, mimea huonesha dalili za kunyauka hata katika hatua ya ujana, huku majani yakigeuka na kuwa ya manjano. Kwa mimea iliyokomaa, unyaukaji kidogo mara nyingi huonekana kwenye sehemu za mimea. Hii ni kawaida zaidi wakati wa saa za joto zaidi za mchana. Majani baadaye huanza kugeuka manjano, mara nyingi upande mmoja tu. Sehemu za ndani za shina kwa urefu zinaonyesha kubadilika rangi kuwa nyekundu-kahawia kwenye tishu za ndani, kwanza kwenye kitako, kisha juu ya shina.
Wakala (Vijidudu) kadhaa wa kudhibiti kibayolojia, ikiwa ni pamoja na bakteria na aina zingine za F. oxysporum zisizo na vimelea vya magonjwa ambazo zinashindana na zile zenye vimelea vya magonjwa, zimetumika kudhibiti mnyauko Fusari katika baadhi ya mazao. Trichoderma viride inaweza pia kutumika kutibu mbegu (10g/kg ya mbegu). Baadhi ya udongo unazuia ukuaji wa Fusari. Kurekebisha pH ya udongo hadi 6.5-7.0 na kutumia naitreti badala ya ammonium kama chanzo cha naitrojeni kunaweza kupunguza ukali wa ugonjwa.
Wakati wote zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaiyolojia ikiwa yanapatikana. Tumia dawa za kuua kuvu/ukungu zinazotumika kwenye udongo kwenye maeneo yaliyoathirika ikiwa hakuna hatua nyingine zinazofaa. Kulowanisha udongo kwa maji yenye copper oxychloride (3g/l) kabla ya kupanda/kupandikiza pia ni njia yenye ufanisi.
Mnyauko wa fusari hukua kwenye tishu za usafirishaji za mimea, na kuathiri usambazaji wa maji na virutubisho. Mimea inaweza kuambukizwa moja kwa moja kupitia ncha za mizizi yake au kupitia majeraha kwenye mizizi. Mara vimelea vya magonjwa vinapokaa katika eneo, vinabaki hai kwa miaka kadhaa.