Uromyces pisi
Kuvu
Mkusanyiko wa chavua za kahawia huonekana pande zote mbili za majani na kwenye mashina. Katika hali ya hewa kavu, mlundikano wa chavua hizo huenea. Majani huharibika umbile na mmea wote unakuwa na ukuaji mdogo. Hata hivyo, mavuno hupungua kwa kiasi kidogo.
Uharibifu hugunduliwa zaidi katika hatua za mwisho za ugonjwa huu. Mara nyingi matibabu sio lazima, kwani upotevu wa mavuno/kipato ni mdogo.
Dawa za kuua kuvu zenye Tebuconazole zinaweza kutumika
Kuvu/fangasi hujificha kwenye maharage shamba(pia hujulikana kama maharage kengele, maharage mapana au maharage ya Kiingereza), pojo na aina za mtongotongo/mnyapa. Kutokea hapo, huenea kwenye mimea ya njegere wakati wa majira ya kuchipua. Kipindi cha majira ya baridi, Kuvu huhamia kwenye mimea mingine mipya ambayo ni mwenyeji.